Romelu Lukaku Ahusishwa na imani za Kishirikina

Mapya yameibuka baada ya moja kati ya matajiri wa klabu ya Everton Farhadi Moshri kuibuka na kutaja masuala ya ushirikina kuwa kati ya mambo ambayo yalimfanya Lukaku kuondoka katika klabu yao.

Farhadi Moshri amesema kwamba kilichomuondoa Lukaku kutoka Everton sio masuala ya kipesa kama inavyoonekana kwani walikuwa tayari kumpatia hadi kiasi cha £140,000 kwa wiki ila alikataa.

Lakini Moshri anadai kwamba mchezaji huyo alikuja Africa ambapo alikutana na ujumbe wa mganga ambao ulimshauri kuondoka katika klabu ya Everton na kutimkia Chelsea ambapo hata hivyo baadae alikwenda Manchester United.

Moshri amesema kwamba masuala yao na Lukaku yalikuwa yakikaribia kabisa kumalizika na hadi wakala wa mchezaji huyo alikuwa akikaribia kumaliza jambo hilo lakini ghafla Lukaku alibadilika.

Tajiri huyo wa Everton pia ameeleza masikitiko yake kuhusu Ross Barkley kwani anaamini wao kama Everton mchezaji huyo ndio waliamini anaweza kubaki nao baada ya Stones na Lukaku kuondoka ila hawakuwa na namna zaidi ya kumuuza kwenda Chelsea.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad