Kamanda wa polisi mkoa wa Iringa, (RPC) Julius Mjengi amefunguka na kuweka wazi sababu zilizopelekea kumkamata Mbunge wa Iringa Mjini, Mchungaji Peter Msigwa na kudai kuwa walimkamata wakimtuhumu kuratibu kuchoma na kubomoa nyumba.
Mjengi amesema hayo leo Januari 23, 2018 wakati akiongea na www.eatv.tvna kudai kuwa Mbunge huyo jana alipokamatwa alihojiwa na baadaye aliachiwa kwa dhamana hivyo yupo huru kwa dhamana toka jana majira ya saa tano usiku.
"Jana Msigwa alijisalimisha baada ya kusikia tunamtafuta hivyo tulimuhoji na usiku alipata dhamana, hivyo sisi tulikuwa tunamtafuta kwa tuhuma za kuratibu matukio mawili ya uhalifu hapa Iringa Mjini ambapo kuna nyumba ya diwani mmoja ambaye alijiuzulu na kuhama CHADEMA na kuhamia CCM nyumba yake pagale lilibomolewa"
Kamanda aliendelea kusema kuwa
"Lakini pia usiku wa kuamia tarehe 17 kuna nyumba moja Kihesa ilichomwa moto ikateketea na ndani mle katika wapangaji mmoja alikuwa ni Katibu wa UVCCM Wilaya ya Iringa Mjini kwa hiyo Msigwa ana tuhuma za kuratibu matukio haya, kwa hiyo tulimuhoji na kudhamini ila tunaendela naye" alisisitiza Kamanda wa polisi mkoa wa Iringa, (RPC) Julius Mjengi
Msigwa usituanzishie fujo na machafuko. Iringa yetu ni Salama na Amani.
ReplyDeleteukitaka kwenda KANDA ile ya kule tafadhali fanya hivyo lakini si hapa kwetu.
siamini kama msigwa anaweza kufanya hili. huu ni uongo na serikali na polisi tafadhali sana mjiangalie kwa haya. kubambikiwa kesi. ni kubaya sana.
ReplyDeleteKwani wakati wote uko naye hadi useme huamini?, na kama si hivyo ujue wanasiasa wanaweza fanya kitu chochote kulinda mikate yao, fungua macho uone.
DeleteMbona hawa wanaoshutumiwa ivi kama ni kweli mbona keai zao huwa zinaisha kimya kimya? Mbona huwa awafungwi polisi na serikali jamani jiangalieni tutawachoka
ReplyDelete