Kufuatia tukio la beki wa klabu ya Kagera Sugar, Juma Nyoso kudaiwa kumpiga shabiki hadi kuzimia baada ya mchezo wao na timu ya Simba hali iliyopelekea kukamatwa na Jeshi la Polisi Mkoani Kagera.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kagera, Agustine Ollomi amesema hali ya majeruhi anaye fahamika kwa jina la Shabani Hussein mwenye umri wa miaka 33 bado ni mbaya na yupo mikononi mwa madaktari huku mtumuhimiwa akiwa sero hado hapo upelelezi utakapo kamilika.
Kamanda Ollomi ameyasema hayo hapo jana mbele ya waandishi wa habari mara baada ya tukio hilo.
Leo kulikuwa na hiyo mechi ya ligi kuu kati ya Simba SC na Kagera Sugar, mechi ilikwenda salama hadi kumalizika kwa timu ya Simba kupata ushindi wa magoli 2-0.
Sasa wa kati wanatoka uwanjani mashabiki walikuwa ni wengi , yuko mmoja anaonekana kama wa Simba alikuwa anapuliza vuvuzela kwahiyo katika kupuliza kwake akawa anampulizia Juma Nyoso mchezaji wa Kagera Sugar ambaye ameshindwa.
Ilikuwa ni katika hali ya ushabiki lakini huyu mchezaji wa Kagera Sugar, Juma Nyoso aligeuka na kumshika yule shabiki akawa amemkunja akampiga futi la mguu akawa amepata jeraha kwenye paji la uso akazimia.
Majeruhi amechukuliwa na kukimbizwa kwenye hospitali ya Mkoa hapa Bukoba kwaajili ya matibabu haliyake bado siyo nzuri kwasababu alipoteza fahamu palepale madaktari wapo wanaendelea kuweka haliyake sawa.
Kamanda Ollomi amesema kuwa kitendo alichofanya mchezaji Juma Nyoso ambaye kwa sasa yupo sero kimevuruga raha ya mchezo huo huku akisema kuwa majeruhi wa tukio hilo anaitwa Shabani Hussein mwenye umri wa miaka 33.
RPC Kagera: Hali ya Shabiki Aliyepigwa na Nyoso Bado ni Mbaya Yupo Mikononi mwa Madaktari
1
January 23, 2018
Tags
mjenge viwanja ambavo masahbiki hawawezi kuingia uwanjani
ReplyDeletenchi nyingine mashabiki wengi huwa wanakufa huku timu imefungwa huku una hasira halafu shabiki akukere lazma mambo yawe tofauti