Serikali: Hatuna Mpango Kurejesha Fedha za Sarafu

Serikali: Hatuna Mpango Kurejesha Fedha za Sarafu
Serikali ya Tanzania imesema haina mpango wa kurejesha fedha za sarafu ndogo kuanzia senti tano hadi shilingi 20 katika mzunguko wa fedha kutokana na ubebaji wake kuwa mgumu.

Hayo yameelezwa na Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Ashantu Kijaji kwa niaba ya Waziri wa Wizara hiyo, leo Bungeni mjini Dodoma (Jumanne) katika mkutano wa 10 wa Bunge kwenye kikao chake cha kwanza wakati akijibu swali la mbunge wa viti maalum, Mhe. Salma Kikwete ambaye alitaka kujua ni kwa nini serikali haioni kuwa ni wakati muafaka kurudisha sarafu hizo katika mzunguko wa matumizi kutokana na kuwapo na bei za shilingi zinazohitajika kuwapo na senti.

"Benki kuu ya Tanzania imepewa kisheria jukumu la kuzalisha fedha za noti sarafu kulingana na mahitaji pamoja na mazingira ya kiuchumi yaliyopo. Mambo muhimu ambayo yanazingatiwa wakati wa kuondoa na kuingiza katika soko noti na sarafu ya thamani ndogo na kubwa ni mfumuko wa bei wa bidhaa za huduma, kulinda thamani na wepesi wa sarafu kubebeka", alisema Dkt. Ashantu Kijaji.

Pamoja na hayo, Dkt. Ashantu Kijaji aliendelea kwa kusema "kwa kuwa hatuna sera ya kupanga bei za bidhaa na huduma kwa sasa ni vigumu kurejesha sarafu hizo katika mzunguko wa fedha kwa njia iliyopendekezwa na Mbunge Salma Kikwete"

Kwa upande mwingine, Naibu Waziri wa Fedha na Mipango amesema sarafu hizo zitaweza kurudi katika mzunguko wa fedha kwa urahisi endapo pale teknolojia ya kufanya miamala ya fedha kwa njia ya mitandao itasambaa nchini kote na jamii kuwa tayari kufanya miamala hiyo kwa njia ya mitandao.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad