Serikali Itawashughulikia Papo Hapo Hatutawaundia Tume- Waziri Majaliwa

Serikali Itawashughulikia Papo Hapo Hatutawaundia Tume- Waziri Majaliwa
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amewataka watumishi wa umma nchini wasijihusishe na vitendo vya wizi, ufisadi kwani Serikali haitosubiri kuwaundia tume za kuwachunguza bali itawashughulikia hapo hapo.

Majaliwa amesema hayo akiwa mkoani Mara Wilayani Musoma na kudai kuwa Serikali haiko tayari kuwavumilia watumishi wanaojihusisha na wizi, ubadhilifu, rushwa na uzembe, hivyo ni vema viongozi waliopewa dhamana wahakikishe wanatekeleza majukumu yao kwa uadilifu.

"Fedha zinazotolewa na Serikali kwa ajili ya utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo zinalenga kutatua kero za wananchi na si kuwanufaisha wachache wenye tamaa. Kama ni za ujenzi wa zahanati ijengwe na atakayezitafuna Serikali haitosita kumchukulia hatua".

 Aidha Waziri Mkuu asiwasisitiza watumishi wa umma kufanya kazi kwa mujibu wa sheria kwa sababu vitendo vya wizi, uzembe vinachangia kupunguza kasi ya kuwaletea maendeleo Watanzania.


Mbali na hilo Waziri Mkuu aliwataka Wakuu wa idara na watendaji wengine wa halmashauri kuacha tabia ya kukaa ofisini na badala yake waende vijijini kwa ajili ya kuwafuata wananchi na kushirikiana nao katika kutatua kero mbalimbali zinazowakabili.

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Swadakta.... No time to waste.
    Tutafika na mtaeleweka. Change of culture and performanca driven.
    Tanzania mpya kwa hivi itakuja tu.
    Hapa kazi tu.

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad