Serikali yafunguka Kukamatwa Meli ya Tanzania

Msemaji Mkuu wa Serikali, Dkt. Hassan Abbas amefunguka kuhusu meli inayodaiwa kuwa na usajili wa Tanzania iliyokamatwa Santo Domingo, Jamhuri ya Dominican siku ya Boxing day ikidaiwa kuwa na madawa ya kulevya aina ya Cocaine yenye ujazo wa tani 1.6

Dkt. Abbas akizungumza leo na waandishi wa habari amekiri kuwepo kwa taarifa hizo na kudai kuwa wao wanaifanyia kazi illi kujua ukweli juu ya sakata hilo ambalo limekuwa likiripotiwa kwa siku kadhaa sasa.

"Suala la meli iliyokamatwa Dominica hili nalifahamu nimelisikia kwa hiyo wenzetu wa Wizara ya Mambo ya Nje bado wanafuatilia kujua usahihi, maana yake imeripotiwa hivyo kwa hiyo Wizara ya Mambo ya Nje tumeshaongea nao wanafanyia kazi kama kutakuwa na taarifa nyingine basi itatolewa" alisema

Taarifa za awali zilikuwa zinasema kuwa Jeshi la Maji la Uholanzi liliishtukia meli hiyo siku ya Christmas na kuikamata siku kesho yake ambayo ilikuwa siku ya boixing day na kuipeleka Santo Domingo, Dominican. Mnamo Disemba 31, 2017 Meli hiyo ilifanyiwa uchunguzi na kubainika kuwa ilikuwa imebeba kilo 1600 ambazo ni sawa na tani 1.6 za madawa ya kulevya zilizokuwa zimefichwa kwenye matenki ya mafuta.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad