Serikali Yakubali Maoni ya Wabunge..... Yafuta Mamlaka ya Waziri, Umri wa Kustaafu

Serikali Yakubali Maoni ya Wabunge..... Yafuta Mamlaka ya Waziri, Umri wa Kustaafu
Serikali imekubali maoni ya Kamati ya Bunge ya Katiba na Sheria ya kukifuta kifungu kilichokuwa kikimpa mamlaka Waziri wa Utumishi na Rais kubadili umri wa kustaafu kwa mtumishi wa umma.

Muswada wa Sheria Mbalimbali Namba 5 wa Mwaka 2017 unapendekeza kufanya marekebisho katika sheria ya utumishi kwa lengo la kubadili umri wa kustaafu kwa baadhi ya kada za utumishi wa umma.

Kada zinazopendekezwa kuongozewa umri wa kustaafu kutoka miaka 55 hadi 60 kwa hiari na 60 hadi 65 kwa lazima ni maprofesa, madaktari bingwa na wahadhiri waandamizi  wa vyuo vikuu vya umma.

Mwanasheria Mkuu wa Serikali, George Masaju amesema bungeni leo Jumanne Januari 30,2018 kuwa kifungu kipya cha 25B ambacho kilikuwa kinapendekeza umri wa kustaafu kimefutwa.

Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Katiba na Sheria, Mohamed Mchengerwa amesema kamati haikuona haja ya kuwa na kifungu hicho kipya kwa sababu kinaweza kutumika vibaya kwa sababu mfanyakazi husika hapewi nafasi ya kushirikishwa katika uamuzi.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad