Serikali imesema haioni sababu ya kuendelea kulumbana na Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu, ambaye, anapata matibabu jijini Nairobi baada ya kushambuliwa kwa risasi Mjini Dodoma takribani miezi minne iliyopita.
Msemaji Mkuu wa Serikali, ambaye pia ni Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo, Dk. Hassan, Abbas, ametoa kauli hiyo kufuatia Mh. Lissu kuituhumu serikali juu ya kushambuliwa kwake na kumsababishia majeraha makubwa mwilinini mwake.
Dk. Abbas kupitia ukurasa wake wa Twitter, amesema, Mbunge huyo bado ni mgonjwa na kwamba Serikali inaendelea kumuombea Tundu Lissu ili apone haraka.
"Mhe Lissu bado ni mgonjwa na yuko wodini hivyo Serikali haioni busara kulumbana naye kwa sasa. Tunaendelea kumuombea apone haraka" ilisema taarifa ya Dkt. Abbas
Tundu Lissu leo Januari 5, 2018 ametoa malalamiko yako na kusema kuwa kitendo cha yeye kupigwa risasi kuwa ni mipango iliyokuwa inalenga kumzimisha kabisaa ili asiendelee kuwasumbua