Uongozi wa kata ya Nyehunge Wilayani Sengerema mkoani Mwanza, umetolea ufafanuzi taarifa za kuwepo kwa sheria ya kuwachapa viboko 12 mtu yeyote atakayekutwa amesimama na mwanafunzi wa kike, na kusema kwamba taarifa hizo hazina ukweli wowote.
Akizungumza na mwandishi wa www.eatv.tv diwani wa kata hiyo Charles Kalam Mbogo, amesema taarifa hizo hazina ukweli kabisa, kwani hakuna kikao cha uongozi wa kata hiyo, kilichopitisha sheria hiyo.
Hivi karibuni kumekuwa na taarifa kuwa uongozi wa kata ya Nyehunge, wilayani Sengerema umepitisha sheria ya kuwachapa viboko 12 au faini ya shilingi 10,000 wanaume wote watakaokutwa wamesimama na wanafunzi wa kike, kufuatia kukithiri kwa tatizo la wanafunzi hao kukatisha masomo kwa sababu ya kupata ujauzito.
EATV.