Shida ni Kwamba Waliosema Mzee Kikwete ni Dhaifu ndio Wanasema Rais Magufuli ni Dikteta

Wakuu,

Tabia aijengayo mtu hujenga taswira yake katika jamii na kufanya matendo yake yatafsiriwe kutokana na yeye alivyo na si kile anachokifanya kwa wakati huo. Kwa mfano, mtu akiwa mwongo Mara kwa Mara, inawezekana siku Akasema kweli lakini kwa kuwa tayari anafahamika ni mtu mwongo, ukweli wake hauwezi kuchukuliwa kwa uzito wowote. Mathalan, mtu anaweza kuwa na desturi ya kudhulumu na kwa mantiki hiyo, hata siku akikuambia kadhulumiwa, itakiwa ni vigumu kumchukulia serious kwa kuwa unajua tabia yake.

Sasa hivi kuna watu wanasema Rais Magufuli ni dikteta, hataki ushauri na hafuati sheria kuamua Lakini shida wenye hoja hiyo ndio waliokuwa na hoja kwamba Mzee Kikwete alikuwa ni Rais dhaifu na ailikuwa hafai.

Walichokuwa wanaona ni kosa kwa Mzee Kikwete, ilikuwa ni desturi yake ya kuwa na tabasamu muda wote kama ishara ya upendo kwa watu, kila lilipotokea jambo alisisitiza vyombo husika viachwe vilifanyie kazi kwa mujibu wa sheria Hata wanaolalamika Leo wakasema wanataka mabadiliko, wakasema wanahitaji Rais Mkali, Rais Mwenye maamuzi magumu na wengine wakaaenda mbali na kusema nchi hii sasa inahitaji dikteta ili ainyooshe.

Sasa basi hoja yangu ni nini? Kimsingi Leadership style ya Rais Magufuli, kwa kiasi ni Opposite ya leadership style ya Mzee Kikwete. Kwa Hiyo tungetaraji wale waliotuambia Mzee Kikwete alikuwa dhaifu ndio wamuunge mkono Rais Magufuli lakini cha ajabu hao hao wengi wao ndio wanaomlaumu.

Hii maana yake nini? Ni mambo mawili. Jambo la kwanza ni amma hatuna uhakika tunachotaka ni nini, amma tuwanafiki wa kiwango cha SG.

Sasa ili tutoke tulipo, ndio maana Mara nyingi sisi wengine tunasisitiza kuwa tuna tatizo kubwa la kijamii. Watanzania kama jamii wengi wetu tuna mitizamo isiyo sawa Mara nyingi. Wengi hatuko focused, hatuko dertamined na si tu kwamba hatuwawazii mema wengine lakini hatujiwazii mema hata sisi wenyewe. Kwa Maneno mafupi tumetawaliwa na negative thoughts na unafikiri mkubwa kama misingi yetu mikuu ya maisha.Mara nyingi hatutaki kusema wala kusimamia ukweli, lakini pengine wana hatuna uhakika ukweli ni upi kwa kuwa hatuna uhakika tunasimamia nini.

Sasa kwa kuwa viongozi wetu wote wanatoka katika jamii hii hii, tutegemee aina ya viongozi tunaokuwa nao ni reflexion ya sisi kama jamii tulivyo, na kama tunadhani tunatakiwa tuwe na viongozi wa aina Fulani, tunatakiwa tu affect the course ambayo ni jamii.

Kweli nawaambieni, Miaka 20 ijayo huenda tukapata Rais ambaye tulikuwa naye humu Jf halafu tutakuwa tunaanza kulaumu hana hiki hana kile hajaandaliwa kimepanda , kimeshuka, ni dhaifu ana roho mbaya n.k

Labda tu niulize, kwa mfano hapa Jf, ni nini kinachosababisha tusijikite kwenye kuleta mada ambazo zinasaidia kuandaa viongozi bora Leo na kesho na hata ikitokea mtu akaleta, wachangiaji hakuna na wakiibuka wachangiaji ni matusi tu ndio input yao.

Jibu ni hili, bado hatujawa na uhakika wa tunachokitaka na hivyo tumeupa nafasi unafiki uwe ndio msingi wetu Mkuu wa maisha. Tusipobadilika tutaendelea kudhani kuwa adui yetu ni Fulani kumbe adui yetu yu ndani ya nafsi zetu wenyewe, na tusipobadilika .........

By Azizi Mussa/JF
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad