Simba imeyaanga mashindano ya Mapinduzi 2017/18 kwa aibu baada ya kutolewa katika hatua ya makundi kwa kufungwa 1-0 na URA katika mchezo wa mwisho wa Kundi A uliokuwa unaamua umu gani kati ya hizo itasonga mbele.
Simba ilikuwa inahitaji ushindi kwenye mchezo huo ili kufikisha pointi saba (sawa na URA) lakini watoto wa Msimbazi wangefuzu nusu fainali kwa tofauti ya magoli.
Kwa upande wa URA wao walikuwa wanahitaji sare tu ili kufikisha pointi nane ambazo zisingefikiwa na Simba kwa sababu wangesalia na pointi tano.
Ushindi dhidi ya Simba unaifanya URA ifikishe pointi 10 na kuongoza Kundi A mbele ya Azam ambao wanapointi tisa.
Katika mechi nne ambazo Simba imecheza katika hatua ya makundi, imeshinda mechi moja pekee, sare moja na kupoteza michezo miwili. Imemaliza katika nafasi ya tatu kwenye Kundi A ikiwa na pointi nne nyuma ya Azam (pointi 9) na URA (pointi 10).
Msimu uliopita 2016/17, Simba ilicheza fainali na kupoteza kwa kufungwa 1-0 na Azam ambao walitangazwa mabingwa.