Simba Yamtangaza Rasmi Kocha Mfaransa Mpya Pierre Lechantre Atakayekinoa Kikosi Hicho

Simba Yamtangaza Rasmi Kocha Mfaransa Mpya Pierre Lechantre Atakayekinoa Kikosi Hicho
Klabu ya Simba leo imemtangaza rasmi Mfaransa Pierre Lechantre, kuwa Kocha mpya atakayekinoa kikosi hicho ambacho kilikuwa hakina mwalimu baada ya kumfukuza aliyekuwa kocha wake, Joseph Omog mwishoni mwa mwaka jana.

Taarifa hiyo iliyotolewa na Msemaji Mkuu wa Klabu hiyo, Haji Manara imeeleza kuwa kocha huyo ataanza kazi mara moja na atasaidiwa na kocha msaidizi wa sasa Masoud Djuma ambae alikuwa akikaimu nafasi hiyo na Mfaransa huyo atashuhudia mchezo wa Simba SC dhidi ya Singida United leo Januari 18, 2018 katika Uwanja wa Taifa.

Mfaransa huyo alishawahi kukinoa kikosi cha timu ya taifa ya Cameroun kilichoshinda ubingwa wa Afrika mwaka 2000 na ameshawahi kushinda tuzo ya kocha bora wa bara la Afrika 2001.

Soma zaidi taarifa hiyo kutoka Simba SC;

                                          TAARIFA KWA UMMA
Klabu ya Simba inayo furaha kubwa kuwajulisha Wanachama na washabiki wake kwamba imempata kocha wake mkuu mpya,Mfaransa Pierre Lechantre.

Kocha huyo mzoefu ataanza kazi mara moja na atasaidiwa na kocha msaidizi wa sasa Masoud Djuma ambae alikuwa akikaimu nafasi hiyo

Kocha Lichantre keshawahi kufundisha vilabu kadhaa duniani kikiwemo kikosi cha Timu ya Taifa ya Cameroun kilichotwaa ubingwa wa Africa 2000.
Kocha huyo pia alipata kuwa kocha bora wa Afrika mwaka 2001 na pia barani Asia mwaka 2012.

Lechantre amekuja pia na kocha wa viungo Mmorocco Mohammed Aymen Hbibi, Na leo jioni kocha Lechantre ataishuhudia Simba ikicheza na Singida United kwenye Uwanja wa Taifa.
IMETOLEWA NA
HAJI S MANARA
MKUU WA HABARI SIMBA SC
SIMBA SC NGUVU MOJA
Tags

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Kwanini asiwe kocha wa timu ya Taifa? Iweje simba iwe na uwezo wa kuleta kocha wa maana na ikashindikana kwa timu ya taifa? Au ndio kusema timu ya taifa haina mwenyewe? Au wale waliokabidhiwa timu ya Taifa hawajui wanachokifanya? Au wanasubiri imebakia wiki moja kabla ya mashindano hakika ndio wanaleta kocha tena kocha mwenyewe kilaza? Au wanasubiri mpaka Magufuli awakurupushe ndio waamke? Kitu ambacho kitaamsha bifu na FIFA. Watanzania tujaribu sana kuiga utendendaji kazi wa Magufuli kwani ni mtu anaefukazana na muda kuhakikisha hakuna kulala katika kutafuta ufumbuzi wa matatizo kwa haraka ili kuleta maendeleo ya haraka. Watu wa TFF inaonekana hawajui hasa nini majukumu yao. Nadhani suala la timu ya Taifa moja ya dhamana zao kubwa kabisa lakini inaweza kupita miezi miwili bila kusikia taarifa zozote zianazohusiana na Timu ya Taifa kama vile ndio kitu cha mwisho kuliko hata DODOMA FC. NA kwanini timu ya Taifa wasipokonywe TFF na ikawa chini ya serikali? Hongereni simba ipo siku mtapatia tu jitihada zenu zinaonekana sana. Tunaimani ipo siku mtatutowa kimasomaso soka.

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad