Simba Yaonyesha Ubabe Wake Mbele ya Kocha Mpya Yaiadhibu Singida United Bila Huruma

Simba Yaonyesha Ubabe Wake Mbele ya Kocha Mpya Yaiadhibu Singida United Bila Huruma
Klabu ya Simba leo imepiga klabu ya Singida United bao 4- 0 katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania bara ambao umechezwa katika uwanja wa Taifa na kushuhudiwa na kocha Mkuu mpya wa Simba Mfaransa Pierre Lechantre.


Katika kipindi cha kwanza cha mchezo mshambuliaji mahiri Kichuya aliweza kuwaamsha mashabiki wa Simba ndani ya dakika ya tatu ya mchezo kwa goli la kwanza la kuongoza ambalo aliweza kulifunga kwa mtindo wa sarakasi na kumpoteza goli kipa wa Singida United Manyika Jr.

Mchezo uliendelea kuwa wa kasi na Simba kuonekana kutawala mchezo na kupelekea kuongeza furaha ya mashabiki wa klabu hiyo baada ya Beki wa Simba Asante Kwasi kuifunga goli la pili Singida United katika dakika ya 23 ya mchezo.

Mpaka wanakwenda mapumziko Simba tayari walikuwa wametangulia kwa goli 2-0 dhidi ya Singida United, katika kipindi cha pili cha mchezo Simba walionyesha uhai na nguvu zaidi ya mashambulizi na kupelekea mshambuliaji wa Kimataifa Emmanuel Okwi kuitandika goli ya tatu Singida United katika dakika ya 75.

Okwi aliongeza goli lake la pili katika mchezo huo katika dakika ya 82 ya mchezo na kupelekea klabu yake kuibuka na ushindi wa bao 4-0 dhidi ya Singida United

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad