Klabu ya Soka ya Simba ya jijini Dar es Salaam, leo mchana imemtambulisha rasmi kocha wao mpya Raia wa Ufaransa, Pierre Lichantre, ili kuanza kuinoa Klabu hiyo baada ya kuachana na aliyekuwa kocha wao, Mkameruni Joseph Omog.
Kocha Pierre Lechantre ametambulishwa leo katika ukumbi wa mikutano wa hotel ya Movenpick jijini Dar es salaam, tukio lililoendana na kusainishana mikataba. Kocha huyo amekuja pamoja na kocha wa viungo Amin Mohamed Habib.Kocha Lechantre amewahi fundisha timu ya taifa ya Cameroon iliyochukua ubingwa wa Afrika.
Klabu ya soka ya Simba ipo mjini Bukoba kujiandaa na mchezo dhidi ya Kagera Sugar Jumatatu. Lechantre ataanza kazi mara moja timu itakaporejea Jumanne baada ya mchezo huo.
Msemaji wa Simba, Haji Manara pia amewashukuru mashabiki wa Simba kwa sapoti ambayo wameionyesha na kuwahkikishia ushindi mpaka watakapochukua ushindi wa ligi kuu. Hii ni mara ya kwanza kwa kocha Mfaransa kufundisha vilabu vya Tanzania.
Lechntre amesema; “Nitajitahidi kufanya kazi na kocha Djuma, kuipigania timu kuipeleka mbele katika mashindano ya Afrika. Nipo hapa kuipigania timu na kumfanya kila mtu awe na furaha katika klabu”
Katika mkutano huo Simba iliwatangaza viongozi walioteuliwa kuongoza kamati ya maadili itakayoongozwa na Mwenyekiti, Suleiman Kova aliyekua mkuu wa Polisi, Robert Selasela, Suleiman Ali aliyekua katibu wa zoezi la kuibadilsha simba kuwa kampuni pamoja na Steven Ali.