Taasisi ya Aga Khan Yazindua Kituo cha Afya Wilaya ya Ilala

Taasisi ya Aga Khan Yazindua Kituo cha Afya Wilaya ya Ilala
Taasisi ya Huduma za Afya Aga Khan Tanzania imezindua  kituo kingine cha afya wilayani Ilala cha Aga Khan Polyclinic.

Akizungumza leo Januari 26, mwaka 2018 katika ufunguzi wa kituo hicho, Mkurugenzi Mtendaji Mkuu wa taasisi hiyo Kanda ya Afrika Mashariki,  Sulaiman Shahabuddin amesema kitakuwa alama kuu ya ukuaji wa uboreshaji wa huduma za afya katika mkoa huo..
"Hiki ni kituo chetu cha tisa katika mkoa wa Dar es Salaam na cha 16 nchini, kituo hiki kitaleta tija ya huduma bora za afya kwa wananchi wa Ilala hasa katika eneo la Ukonga na Gongo la Mboto,” amesema.

Mganga Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Dk Grace Magembe amesema, “Naelewa tafsiri nyingine kubwa ya uwekezaji mnaofanya mbali na kuongeza  nafasi kuchagia ukuaji wa kasi wa huduma bora, salama na nafuu za afya kwa Watanzania pia mnafungua  milango ya ajira.”
Kituo hicho kitatoa huduma za afya ya mama na mtoto, kliniki za watoto na kinamama, ultrasound, X Ray na vipimo vya awali vya moyo.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad