Taharuki Yazuka Mtwara Wakesha Wakinywa Uji kwa Kutekeleza Agizo la Mtoto Aliyezaliwa na Kuongea Papo Hapo

Taharuki Yazuka Mtwala Wakesha Wakinywa Uji kwa  Kutekeleza Agizo la Mtoto Aliyezaliwa na  Kuongea
Katika hali isiyo ya kawaida, baadhi ya wakazi wa maeneo mbalimbali mkoani Mtwara na maeneo mengine ya mikoa ya jirani wamejikuta wakikesha nje ya nyumba zao usiku wa kuamkia leo Januari 10, 2018, wakipika na kunywa uji utokanao na unga wa muhogo.

Wakazi hao wamedai kuwa wanatekeleza agizo la mtoto mdogo aliyezaliwa katika kijiji cha Mchichira kilicho kati ya nchi ya Msumbiji na mkoa wa Mtwara na kisha papo hapo kuanza kuzungumza.

Imedaiwa kuwa mtoto huyo alisema kuwa mvua ya maajabu yenye sumu itanyesha katika maeneo hayo na ili kujikinga nayo, watu wanapaswa kunywa uji huo kwa Imani kuwa uji huo utazuia kabisa mvua hiyo ya ajabu.

Licha ya kuwepo kwa taarifa za kutatanisha kuhusu ukweli wa jambo hilo, watu waliendelea kuamshana usiku wa manane kunywa uji  huo.
Tags

Post a Comment

3 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. wonders shall never end

    ReplyDelete
  2. shetani yupo kazini! Ndugu zangu tumuombe Mungu tuulize je wewe ni Mungu wa Ibrahimu,Isaka au Israel tunaomba utudhihilishie. Ilibidi wakeshe kwa kuomba sio vinginevyo. Uepuke uovu nao utakuepuka. Zipime roho zinazowajia kimiujiza. Muulizeni Muumba wenu kuhusu hii kitu.

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad