Tanzia: Mwanamuziki Mkongwe Afrika Kusini Hugh Masekela Afariki Dunia Baada ya Kuugua Saratani ya Tezi Dume

Tanzia: Mwanamuziki Hugh Masekela Afariki Dunia Baada ya Kuugua Saratani ya Tezi Dume
Hugh Masekela, mwanamuziki maarufu wa mtindo wa jazz kutoka Afrika Kusini aliyechangia juhudi za kukabiliana na utawala wa ubaguzi wa rangi nchini humo, amefariki dunia akiwa na miaka 78.

Familia ya mwanamuziki huyo mcheza tarumbeta, kupitia taarifa, imesema Masekela amefariki akiwa mjini Johannesburg baada ya kuugua saratani ya tezi dume kwa muda mrefu.

Masekela alipata umaarufu mkubwa kutokana na mtindo wake wa kipekee wa Afro-Jazz na vibao vilivyokuwa maarufu kama vile Soweto Blues.

Wimbo huo alioutoa 1977 ulihusika sana katika harakati za kupambana na utawala wa ubaguzi wa rangi nchini humo.

Amekuwa akitambuliwa na wengi kama "baba wa Jazz nchini Afrika Kusini.
Alisaidia kutumbuiza wakati wa ufunguzi wa michuano ya Kombe la Dunia 2010 Afrika Kusini na mwanamuziki mwenzake Femi Kuti
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad