“Ndugu mteja katika kuboresha usajili wa laini za simu alama za vidole zitatumika kuanzia Februari 5, 2018. Kwa mawasiliano zaidi tembelea maduka yetu,” ni ujumbe ambao watumiaji mbalimbali wa mitandao ya simu nchi wametumiwa kuanzia juzi kutoka katika mitandao yao.
Kuhusu ujumbe huo, Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), imesema kuwa imetoa kibali kwa makampuni ya simy nchini upya kadi za simu kwa kutumia teknolojia ya kisasa ya kielektroniki inayohusisha uchukuaji wa alama za vidole.
Hayo yalisemwa jana na Kaimu Meneja Mawasiliano kwa Umma wa TCRA, Semu Mwakyanjala na kuwatoa hofu wananchi kwamba tayari walishafanya majaribio kuhusu mfumo huo na kuona unafaa.
Alisema kuwa, mfumo huo unatumia alama za vidole na picha ni wenye uhakika ambao ni vigumu kughushi.
“Huu ni usajili wa kielektroniki ambao unaiwezesha kampuni na mamlaka kupata taarifa mbalimbali za mteja kwa muda mfupi.”