TFF Yatoa Onyo Kali Upangaji Matokeo Ligi Daraja la Kwanza

TFF Yatoa Onyo Kali Upangaji Matokeo Ligi Daraja la Kwanza
Moja kati ya kosa kubwa katika mchezo wa soka ambalo linaweza kugharimu timu, kiongozi, mchezaji au refa ni ishu nzima ya upangaji wa matokeo ya mechi, adhabu za upangaji wa matokeo mara nyingi hutolewa kubwa ili kukomesha tabia hiyo na haishangazi ukisikia mtu kafungiwa maisha.

Jumamosi ya January 13 Tanzania zitachezwa baadhi ya game za Ligi daraja la kwanza ambazo zitaamua ni timu ipi na ipi zitapanda kucheza Ligi Kuu msimu wa 2018/2019, hivyo baada ya Ligi daraja la kwanza kuwahi kutuhumiwa kuwa tabia ya upangaji wa matokeo TFF limetoa onyo.

Kama utakuwa unakumbuka vizuri refa Joseph Lamptey raia wa Ghana ni mmoja kati ya marefa wahanga wa vitendo vya upangaji wa matokeo, March 20 2017 Lamptey alitangazwa kufungiwa maisha na FIFA kujihusisha na soka baada ya kubainika kujihusisha na upangaji wa matokeo wa game ya Afrika Kusini dhidi ya Senegal ya kuwania kufuzu World Cup 2018.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad