Tido Mhando Aachiwa Huru kwa Dhamana.

 Tido Mhando Aachiwa Huru kwa Dhamana.
Aliyewahi kuwa Mkurugenzi wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC), Tido Mhando ameachiwa huru baada ya kutimiza masharti ya dhamana.

Tido amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam leo, akikabiliwa na makosa matano yakiwamo matumizi mabaya ya madaraka na kuisababishia serikali hasara ya zaidi ya Sh milioni 800 akiwa TBC.

Wakili wa Serikali, Leonard Swai amedai Tido akiwa Mkurugenzi wa TBC, aliingia mkataba na Kampuni ya Channel 2 Group bila kutangaza zabuni kinyume cha sheria na kuisababishia hasara ya kiasi hicho cha fedha shirika hilo.

Baada ya kusomewa mashtaka hayo na Hakimu Victoria Nongwa alisema dhamana kwa mshtakiwa huyo iko wazi ambapo alitoa masharti ya dhamana kuwa na wadhamini wawili wataosaini bondi ya Sh  milioni 500 kila mmoja.

Aidha, amesema mshtakiwa huyo hatakiwi kusafiri nje ya nchi bila kibali cha mahakama ambapo pia alimtaka kuwasilisha hati yake ya kusafiria mahakamani hapo, kulipa nusu ya fedha iliyopotea na kuwasilisha hati ya mali isiyohamishika. Kesi hiyo imeashirishwa hadi Februari 23, mwaka huu.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad