Tume ya Uchunguzi Yajipanga Kumuhoji Trump

 Tume ya Uchunguzi Yajipanga Kumuhoji Trump
Wanasheria wa Donald Trump wako katika mazungumzo na maofisa wanaoendesha uchunguzi kuhusu Urusi ilivyoingilia uchaguzi ambao wanataka kumhoji rais huyo wa Marekani.

Gazeti la Washington Post likimnukuu mtu ambaye hakutajwa jina lakini akidaiwa kuwa karibu na Trump, limesema kuna uwezekano ofisa anayeongoza uchunguzi huo Robert Mueller akamhoji Trump ndani ya siku chache zijazo. Timu ya wanasheria wa Trump imethibitisha ripoti hizo.

Japokuwa Rais Trump ameeleza kuwa yuko tayari kumpa ushirikiano Muller, wanasheria wake wamekuwa wakijaribu kuhakikisha kwamba mahojiano baina ya ofisa huyo na Trump yanawekewa mipaka maalumu.

Awali taarifa hizo zilitolewa na shirika la habari la NBC, baadaye vyanzo muhimu vililifahamisha gazeti la Washington Post kwamba kuna uwezekano wa Mueller kumhoji Trump hivi karibuni. Ikulu inahangaishwa na uchunguzi wa Mueller kwa sababu hakuna aliyeamini kuwa uchunguzi wake ungeendelea hadi mwaka 2018.

Mueller anachunguza juu ya uwezekano wa kufanyika njama kati ya timu ya kampeni ya kampeni ya Trump mwaka 2016 na Urusi katika uchaguzi wa Marekani.

Wasiwasi kati ya Mueller, mwanasheria aliyeteuliwa kuchunguza juu ya uwezekano wa Urusi uchaguzi, na rais umeongezeka baada ya uchunguzi huo kuwanasa maofisa kadhaa waliopata kuwemo kwenye timu ya kampeni ya Trump.

Utawala wa Trump umekuwa ukikanusha kushirikiana na Urusi wakati wa uchaguzi na rais ameubatiza uchunguzi huo kuwa wa “kusaka mchawi”.

Kwa mujibu wa Washington Post, Muller alidokeza kwa mara ya kwanza juu ya uwezekano wa kumhoji Trump katika kikao na wanasheria wake John Dowd na Jay Sekulow, Desemba mwaka jana.


Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad