Tunda Man Akwaa Skendo Mpya Adaiwa Kutapeli Mamilioni

Tunda Man Akwaa Skendo Mpya Adaiwa Kutapeli Mamilioni
MSANII wa Muziki wa Bongo Fleva zao la Tip Top Connection, Tunda Man anadaiwa kutapeli mamilioni ya urithi ya msanii chipukizi, Asala Kipengele ‘Asala’.

Akizungumza na Full Shangwe, Asala alidai alitapeliwa fedha za urithi Milioni 30 alizompa Tunda Man ili amsaidie kimuziki lakini hadi sasa wamerekodi wimbo mmoja wa Subiri.

“Sitaki kumsikia Tunda kwa kile alichonifanyia, kanipiga sana hela za urithi kwa kujifanya meneja wangu lakini kumbe alikuwa amepanga kunitapeli,”alidai Asala na kuongeza;

“Kuna pesa kama milioni 30 ambayo nilimpatia kwa ajili ya muziki wangu lakini mpaka sasa sielewi chochote hata nikimpigia simu nyingi ni subiri, subiri.”

Full Shangwe lilimtafuta Tunda kujibu madai hayo alidai kwamba si kweli kwamba ametapeli hizo milioni 30.

“Hilo suala ndio nalisikia kwako wala mimi sijatapeli hizo milioni 30 unazoniambia.”
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad