Tundu Lissu Aitaka Jamii ya Kimataifa Kuingilia Kati Tanzania

Tundu Lissu Aitaka Jamii ya Kimataifa Kuingilia Kati Tanzania
Mnadhimu mkuu wa chama cha upinzani nchini Tanzania Chadema Bw Tundu Lissu amesema dalili zinaonesha watu waliomshambulia kwa risasi mjini Dodoma mwaka jana walikuwa na uhusiano na serikali.

Bw Lissu, akihutubia wanahabari kwa mara ya kwanza tangu kulazwa hospitalini, ameonekana kuilaumu serikali ya Rais John Magufuli kwa kuwakandamiza wapinzani.

Amesema anaamini shambulio dhidi yake lililenga kumnyamazisha kutokana na uokosoaji wake wa mara kwa mara wa serikali.

Bw Lissu alikuwa akihutubu kutoka hospitali ya Nairobi jijini Nairobi ambapo amekuwa akipokea matibabu kwa miezi minne sasa.

Mbunge huyo wa Singida Mashariki ametoa wito kwa jamii ya kimataifa kuingilia kati akisema hali nchini Tanzania imebadilika sana.


Bw Lissu amesema kufikia sasa anaamini hakuna uchunguzi wa maana kuhusu kushambuliwa kwake mnamo 7 Septemba unaendelea.

Aidha, amesema Rais John Magufuli, ingawa aliandika ujumbe kwenye Twitter na pia kumtuma makamu wake Samia Suluhu Hassan, hajawahi kuzungumzia hadharani kisa cha kushambuliwa kwake.

"Tanzania imebadilika na kuwa taifa ambalo hakuna aliye salama. Mawakili wanaweza kurushiwa mabomu kwa kuwawawkilisha wateja wao. Nchi ambayo afisi za mawakili zinaweza kuvamiwa, na mawakili kufungwa jela," amesema Lissu.

Bw Lissu amesema amepona na kwamba anashukuru Mungu na wote waliomtakia uponaji wa haraka.
Tags

Post a Comment

2 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Lissu Umekuwa nani wewe hata mpaka Mh Raisi azungumziae Lissu hadharani?
    Wewe ni Mbunge ambao majambazi walikufata na kutaka kuiba.
    Kama hivyo Mh Raisi atakuwa hana kazi nyingine awe anawatembelea wagonjwa na kusimama jukwaani
    kuelezea hali Zao..
    Naona dawa zinafanya kazi yake.
    Dua na sala tunakufanyia. na wewe Jitulize usitafute ya wanahabali na wahalili
    watazidi kukutia malazi. Rudi hospitali ya Rufaa hata mzeee kingunge pia yupo na watanzania wengi tu wanapata matibabu kama kawaida.
    Kama unapesa nyingi za Posho kwa ajili watu wa singida wamekupa ubenge basi endelea kuwawakilisha kwa Nizamu na weledi. Kwani mzee kingunge si bado yuko Hospitali na kapata Msiba mzito. Lakini ni Mzalendo na ana imani na Tiba na Ni Mzalendo.
    Ugua Pole.

    ReplyDelete
  2. Hizo habari za Lisu na Chadema kukimbilia jumuiya za kimataifa hazikuanza leo. Tundu Lisu siku zote amekuwa akihangaika kuipaka matope nchi yetu katika jumuiya za kimataifa kwa kisingizio cha demokrasia. Hata kabla hajapata yaliyompata Tundu Lisu siku zote amekuwa ni mwanaharakati ambae anaepigania kuipaka matope Tanzania katika jumuiya za kimataifa. Tanzania tulikuwa na tatizo la uongozi hasa kiongozi mkuu wa nchi atakaekuwa na uthubutu wa kukemea maovu yaliokuwa yamekithiri nchini hasa rushwa na uvivub kwa watanzania bila ya kupepesa macho. Na la kushangaza zaidi hao akina Lisu na wenzake wakati wakilalamika juu ya uongozi katika awamu ya nne ya kikwete kwamba raisi alikuwa mpole mno kiasi cha wapinzani waliokuwa wakiongozwa na hao akina Lisu kuthubutu kusema yakwamba nchi ilipofikia ilikuwa inahitaji kiongozi wa nchi mwenye uthubutu wa Dikteta. Kwakuwa watanzania wengi ilishafika mahala ambapo mtu akipewa jukumu la kusimamia zamana fulani asipojinufaisha yeye mwenyewe binafsi watu wanamuona mzembe katika jamii iliyomzunguka.Kama tulikuwa tunashida ya kiongozi wa kutuongoza na kututoa hapa tulipo, Magufuli ana kila sifa za kuwa kiongozi huyo sasa kwanini tusimpe muda na ushirikiano wa kutimiza majukumu yake ? Kwanini tuanze kampeni za uchaguzi wa raisi 2020 mara tu baada ya raisi kuapishwa? Maandamano mikutano ya hadhara kwa muda wa miaka mitano ni ya kazi gani? Kwa umasikini wa nchi yetu kweli tunahitaji muda mwingi wa kukusanyika tukisikiliza ahadi hewa kutoka kwa wanasiasa au tunahitaji muda mwingi wa kuwahimiza watanzania kufanya kazi? Kwa hivyo lengo kuu la upinzani sio kuwaletea watanzania maendeleo bali lengo lao kuu ni kukamata madaraka ya nchi hata kwa gharama ya kuhakikisha nchi ina katika vipande vipande? Umoja ni kitu muhimu sana hasa katika wakati wa wapambano na kwa kutambua hili viongozi wengi hasa katika nchi zinazoendelea huwa wakali sana kuhakikisha wananchi wao wanabakia kuwa kitu kimoja. Ni adui pekee atakaekuwa anatamani kuona umoja wa watu fulani walioungana au kuunganishwa kwa ajili ya kujiletea maendeleo unasambaratika. Upinzani wa siasa nchini hasa wa Chadema na washirika wake una kila dalili ya kuchukizwa na umoja na utulivu pamoja na mshikamano waliyonao watanzania katika kuhakikisha muheshimiwa raisi anatimiza majukumu yake. Nafikiri Chadema kwa kutambua ugumu wa kuwashawishi watanzania kufuata siasa za zao ubinafsi ndipo sasa suala la kumwaga sumu katika jumuiya za kimataifa kuipaka matope Tanzania linapokuja. Wapumbavu wanafikiri hao watu wanaokwenda kujipendekeza ni malaika. Wacha tusubiri na tuone hatima yake itakuwaje katika hizo harakati za kwenda kuishitaki Tanzania kwa hao watoa haki? Kwani tulishashuhudia haki za mamilioni ya watu zikibatilishwa kwa matakwa yao binafsi. Ila bila shaka yeyote ile harakati zote hizo za kukimbilia jumuiya za kimataifa ni jitihada za dhati kabisa za kumuhujumu Magufuli ili ashindwe kutekeleza majukumu yake ya kazi hasa yale ya kuhakikisha Tanzania inaondokana umasikini. Binafsi sidhani kama Lisu kapigwa kisiasa na kama kweli waliotaka kumua Lisu walikuwa na bifu la kisiasa basi Tundu Lisu kama akili zake zinafanya kazi vizuri ni wakati wakujitathmini kwani watanzania raisi sana kutenda unyama kwa kujipatia mali iwe hela au hata wivu wa mwanamke lakini watanzania hawajawa wakatili kumtoa mtu roho kwa siasa na kama kitu hicho kikitokea basi ujue pana jambo. Jambo jengine Magufuli si watanzania. Maghufili is an international icon especially in Africa. Waafrica wengi wa mataifa mbali mbali wanamchukulia Maghufili kuwa ndio muarubaini wa matatizo ya uongozi barani Africa. Maghufili ni matumaini ya waafrica wengi. Maghufili ana sapota ya wakereketwa wanaomsapoti wengi zaidi nje ya Tanzania kuliko watanzania wenyewe. Kwa hivyo kutafuta bifu na Magufuli sio jambo busara hata kidogo kwani ni kujijengea uhasama na uadui barani Africa na kwengineko. Waafrica wengi bado wanajiuliza ilikuwaje waliwapoteza kizembe akina Tomas Sankara na mashujaa wengine? Jibu waafrica wasingependa yakina Sankara yatokezee katika new generation yaakina Magufuli.

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad