HALI ya Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu inaendelea kuimarika huku akiendelea na mazoezi ya viungo katika Hospitali ya Nairobi nchini Kenya ambako anapatiwa matibabu ya majeraha aliyoyapata baada ya kushambuliwa kwa risasi nyumbani kwake Area D, mjini Dodoma mnamo Septemba 7, 2017.
Akizungumzakatika mahojiano maalum na Kituo cha Runinga cha Azam TV, Lissu ameeleza namna alivyoshambuliwa huku akisema kuwa watu waliotekeleza tukio hilo la kinyama dhidi yake aliwaona japo hawajui,” alisema Lissu.
Watu walionishambulia kwa risasi niliwaona lakini siwafahamu, nilikuwa nina jitambua mpaka muda nafikishwa Hospitali ya Dodoma, na mtu wa kwanza kumpigia simu alikuwa ni Mwenyekiti wangu wa Chadema, Freeman Mbowe. Dereva wangu ndiye alinisaidia kuwasiliana naye pamoja na watu wengine kuwapa taarifa hizo.
Aidha Lissu amewashukuru madaktari wa Dodoma na wa Hospitali ya Nairobi kwa kufanya jitihada zao kuokosa maisha yake.
“Nisingefika Nairobi bila msaada wa kwanza wa Madaktari wa Dodoma, nilipofika Nairobi Hospital madaktari walifanya kazi kubwa sana kunitibu na kuokoa maisha yangu hadi kufikia hapa nilipo leo.
Madaktari wametoa risasi 16 mwilini mwangu tangu nimefika hapa Hospitali ya Nairobi, risasi moja bado ipo mwilini na risasi zingine 16 zilinikosa siku hiyo ya tukio,” alifafanua Lissu.