Mkuu wa Wilaya ya Kiteto Mhandisi Tumaini Magesa amesema suala la kuwapa mimba wanafunzi limekuwa na utata kwenye sheria, lakini sasa wamegundua njia mbadala ya kuwabaini wahusika wanaokatisha masomo ya wanafunzi.
Akizungumza kwenye kikao kazi cha kukutana na watendaji wa serikali, Mhandisi Magesa amesema njia ya kisayansi ya kupima vinasaba itatumika kuwabaini baba wa watoto hao, na kuwachukulia hatua za kisheria.
'Watu wa DNA wanakuja hapa, tunasubiri tu wale watoto wajifungue halafu sisi tuthibitishe kwamba DNA yako na yule mtoto ni wewe”, amesema Mhandisi Magesa
Mkuu wa Wilaya ya Kiteto amaefikia uamuzi huo baada ya kuwepo na taarifa za kuwepo kwa wanafunzi 159 waliopewa ujauzito na kukatisha masomo.