Wananchi Jimbo la Zitto Waililia Serikali


Mji wa Kigoma ujiji hauna huduma ya maji kwa siku tano sasa baada ya mamlaka ya maji safi na taka kukatiwa umeme na kushindwa kutoa huduma.

Hali ambayo imesababisha wananchi kuhangaika usiku na mchana kutafuta maji maji ya chemchem na visima, na kuiomba serikali kuhakikisha tatizo hilo linakwisha mapema ili kuepuka maradhi wanayoweza kuyapata, kutokana na ukosefu wa huduma ya maji ambayo sasa wanalazimika kutumia maji yasiyo salama.

Akizungumzia hali hiyo kaimu Mkurugenzi wa mamlaka ya maji safi na taka Kigoma Ujiji  Mhandisi Mike Jones, amesema sababu ya kukatiwa umeme ni kutolipa kwa wakati ankara za umeme lakini suala hilo linashughulikiwa haraka ili kuweza kutatua suala hilo
Tags

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Zito amesafiri kwenda mjini twits nchini fwezibooku.
    Ya wana kigoma na ujiko kawaachia wenyewe

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad