Wananchi wana hali ngumu ya maisha – Mhe. Freeman Mbowe

Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa, Mhe. Freeman Mbowe amesema kuwa maisha ya Watanzania yamekuwa magumu kuliko katika kipindi chochote katika historia ya Tanzania.

 Mhe. Mbowe amesema hayo leo jumapili Desemba 31, 2017 jijini Dar es Salaam wakati akizungumza na Waandishi wa Habari.

“Sio siri maisha ya wananchi yamekaza, mimi nimezunguuka nchi hii mikoa mingi, Wananchi wana hali ngumu ya maisha kuliko kipindi chochote katika historia ya nchi yetu,“amesema Mhe. Mbowe huku akifafanua kauli ya kupigwa marufuku kwa matumizi ya neno la vyuma vimekaza.

“Bwana mkubwa hataki neno hili kutumika anasema neno Vyuma vimekaza hataki litumike, Bwana mkubwa yeye vyuma vyake havijakaza kwa sababu halipi umeme, halipii nyumba ya kulala kwa sababu anafanyiwa kila kitu na serikali kwa kodi zetu.“amesema Mhe. Freeman Mbowe.
Tags

Post a Comment

6 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Ulizoea Dili.
    Magu kafunga Dili Zote.
    Flee mani ulie Tu.
    Mbona Mimi naishi na niko poa Tu.
    Mishjaki yangu nikimaliza kuuza usiku naingiza faida baada ya mtaji WA mkaa pilipilina nyanya na ukwaji na kabechi na ndimu.
    Taifa rupu napata kama laki na usher.
    Siku ya pili tunakula na mengine mengi tunafanya.
    While sins wasiwasi Labda igonjwa.
    Maguduli endelea kuwainesha hawa Mafisadi cha myemakuni

    ReplyDelete
  2. Mr Mbowe hali ngumu ilikuwepo miaka mingi ila tu iliwahusu watu wa aina fulani tu. Kinachotakiwa ni mapebdekezo yenye evidence juu ya nini kifanyike kt kuuboresha zaidi uchumi wetu ili kuuboresha standard ya maisha. Nimeipenda zaidi ile plan ya Mr Lipumba Re:mjadala unaolenga kutafuta solution, maana naiona ni more constructive

    ReplyDelete
  3. Sasa kama wananchi wana hali ngumu ya maisha suluhisho ni nini? Je mtu au jamii inapofikwa na changamoto za kimaisha kama kiongozi kukimbilia kulalama ndio suluhisho? Hawa wanasiasa wetu wakati mwengine ni wapumbavu sio ajabu kuona vyama vyao vinakufa. Mbowe na wapambe wake wa upinzani ni opportunist politicians. Ni wanasiasa wanaombea mabaya kutokea nchini kama mtaji wa kisiasa. Mazuri mengi na makubwa kiasi cha kutofikirika kama ingewezekana kufanyika lakini yamefanywa na serikali ya Magufuli tangu aingie madarakani lakini hatujawahi kumsikia Mbowe sio kusifia lakini angalau kuunga mkono kwa hivyo ni dhahiri kwa Mbowe kuyabeza yale yote mazuri yanayoendelea kufanywa na Serikali ya Magufuli na kukimbilia kutoa lawama tu bila ya kutoa suluhisho lolote kwa yale anayolalamikia ni ushahidi tosha kuwa ni mtu mwenye roho mbaya na ubinafsi ambapo kama watanzania watawachekea watu aina yake basi ni hatari ya kujijengea misingi ya maafa zaidi katika maisha yao. Matatizo ni fursa lakini sio fursa ya kutengeneza matatizo zaidi. Hata tiba bora na madaktari bingwa walikuja kupatikana kwa tiba walizolazimika kuzifanya katika mazingira ya vita. Sidhani kama madaktari hao walianza kulia au kupiga makelele ili majeruhi apone? Ninaimani madaktari hao kitendo cha wao kujua kuwa wanafanya kazi katika mazingira magumu kama ya vita ndicho kitu kilichowasukuma kufanya kazi kwa bidii na speed na ubunifu zaidi na matokeo yake tunaambiwa tabibu nyingi za maana hasa za operesheni zilivumbuliwa vitani. Leo hii sisi tuna viongozi wa watu wa vyama vya siasa wanapita mitaani na kukusanya vyombo vya habari na kuanza kuwahimiza wananchi kulia kuwa hali ya maisha ni ngumu? Ukeshaanza kiongozi wa watu kulia lia hovyo je unawaongoza wafanye nini? Kwa viongozi mahiri wanaojitambua huu ni wakati wa bahati kutokea katika maisha yao ya kazi kama kweli kama anavyodai Mbowe kuwa hali ya maisha ni ngumu, kwani ni wakati wa wao viongozi kuwathibitishia kwa vitendo wanaowaongoza kuwa hawakukosea kuwachagua kwa kuonesha uongozi wao kwa kuwaongoza wananchi katika kutafuta ufumbuzi wa changamoto za maisha zinazowakabili na sio kiongozi kulialia hovyo kama kinda la ndege. Vipi kiongozi wa watu awahimize wananchi wake kulia na hali ngumu ya maisha katika nchi ambayo mimea ya vyakula inajiotea wenyewe kabla hata ya kuoteshwa? Kama watu wa kukata au kukatishana tamaa ya maisha wangekuwa Wanyarwanda baada ya kuuwana karibu kumalizana lakini wakaibuka na kuja kuwa strong than ever before. Labda akina Mbowe na wenzake hakuna kingine wanachokitafuta isipokuwa Tanzania kuwa na mfumo wa siasa na kiutawala kama wa Rwanda.

    ReplyDelete
  4. kwa hiyo, Raisi awachie mafisadi, waendelee kutufisadi tu, wao waendelee kuwa matajiri na khali na maisha ya kifshari na masikini waendelee kutabikatu, wakienda hospital madawa hakuna, shule mbovu mbovu tu kama za Kina kayumba, mafisadi holiday Dubai, shopping Dubai, maisha Yale kwa tu, loooo tumewachoka hao watu wa dizaini hiyo katika Taifa hili, Raisi fanya kazi yako, wenginevijipato vyetu ni vya kihalali kabisa, tunajionea sawa tu, huko nyuma ilikuwa hivyo hivyo hata Sasa hivyo hivyo, mijitu mweusi michoyo sana inapenda kuwaibia wenzao tu alafu waishi maisha ya kifahari na kunyanyasa wenzao, ambao wanaowaina masini mpuuuu, mwisho wenu umefika, mkajambe kuleeee. Hapa kazi tu, fanya kazi upate kipato chako halali

    ReplyDelete
  5. Jilani yangu yeye ni muuza nyanja, bamia nyanja chungu, ndizi mshale, yeye kwake maisha ni Yale Yale, kwa hayajui maisha mepesi au magumu, vyuma vimeka au havijakaza, Hauchi kumekucha, hana sehemu ya kupiga dili wala kufanya ufisadi wala kuomba rushwa kwa kuwa yeye Sio mfanyakazi serikalini au TRA hiyo maisha ya kifahar atayajulia wapi, ila jilani wa upande wa pili yeye ni mfanyakazi wa TRA Looooh!!!!!! Anauchukia kweli uongozi wa Sasa kwa kuwa maisha yalikula kwake, mtaani tajiri yeye, majumba ya kifahari kayapanga ndani geit lake, hata mjilani wengine ambao tujumba twa umasikini anawaona ni michosho tu kuwa nao karibu, na haupendi uongozi wa Sasa mpka basi, ukimuona ni kama mtu aliechanganyikiwa muda mwengine anaongea pekee yake huku kichwa kakinamisha chini na mikono nyuma, Manila tukimwangalia tunajua Tatizo lake vyuma vimekaza, na ana hasira huyo wachaaa, angalau ana mlolongo wa Mali alizojilimbikizia kwa rushwa, wizi, ufisadi na kupiga dili, zimejaa Lakini halidhiki na wala hatosheki, Sasa sijui binadam wa hivi tuwaweke kwenye kundi gani? Majilani zake sisi hatuna vyanzo vya kupiga hayo madili vipato vyetu ni vile vile lazima tufanye kazi ndio tujingizie kipato, sisi kwetu furaha yetu ni kuona serikali yetu inatujali katika huduma muhimu, kama huduma za afya, madawa, shule, kwa kile tunacholipia kodi, Sio ziibwe na wenzetu wachache alafu walio wengi wanatabika, tena basi jilani mwenyewe hata shule hana kivile darasa la saba tu, Lakini ndio amekuwa tajiri wa mtaaa, huko nyuma alikuwa hana chochot, Lakini alipowekwa kwenye hiyo kazi ya TRA kipindi hicho hoooo kawa tajili, na akajitahidi kuwekeza na miradi utajili ukaongezeka, na mwengine wa kupiga dili, dili zimekuwa tabu anachanganyikiwa, wakati mtu umewekeza na kuwekeza kwa hela za wizi, kuna binadam wachoyo sanaa na wabaya sanaaa, wanapenda wapate waooo tu na wenzao wawe masikini wawalambe miguu yao, Baba Magu hongera, wote tuwe sawa

    ReplyDelete
  6. Huyu jamaa ni stupi, Idiot, watu wameamka sasa wanawapata wajinga wajinga wenzao, hivi katika hii Tanzania kuna kipindi kilichukua afadhali kwa ille kundi la kawaida na lililokosa sehemu kufisadi, kuiba kupiga diri, Zaidi ya mlo mmja, kibanda kinamatobo shuti kinachuja kama chujio, hayo ndio maisha ya Watanzania wengi toka huko nyuma, miaka yote, tusidanganyane hapa, Mambo ya ulaji upigaji dili ambao ulikuwa unafwanywa na wachache, Raisi aendelee kukomesha kabisa, kama si kusalambatikaaaaaa kabisaaaaa, lingalie kwanza,

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad