Wanaomba Rushwa ya Ngono Kukiona cha Moto


Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Dk Ashatu Kijaji amesema wizara yake imeanza kuchukua hatua kali za kisheria kwa watumishi wa taasisi za elimu ya juu wanaotumia wadhifa wao kuomba rushwa ya  ngono  kwa wanafunzi na kisha kuwapa alama za juu za ufaulu tofauti na uwezo wao kitaaluma.

Dakta kijaji anatoa angalizo hilo jijini Arusha alipokua akizungumza watumishi na wajumbe wa Baraza la wafanyakazi wa chuo cha Uhasibu cha Arusha.

Akizungumza kwa niaba ya watumishi hao makamu Mwenyekiti wa Baraza la wafanyakazi Juma Kaniki akaahidi kuhakikisha maadili yanasimamiwa huku akitumia fursa hiyo kuiomba serikali kuongeza idadi ya watumishi.

Mkuu wa wilaya ya Arusha Gabriel Daqaro aliyeambatana na Naibu Waziri akawakumbusha wajumbe wa Baraza la wafanyakazi kuepuka kuwa chanzo cha migogoro ndani ya taasisi.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad