Wanaume Tata Wamtolea Udenda Idris

Wanaume Tata Wamtolea Udenda Idris
WANAUME tata wameonekana kumtolea udenda Mshindi wa Shindano la Big Brother ‘Hot Shot’ 2014, Idris Sultan baada ya kuposti picha yake kwenye mtandao wake wa kijamii wa Instagram akiwa amevaa nguo ya ndani tu, huku wanaume tata hao wakiweka miguno kwenye picha hiyo.

Kitendo cha wanaume tata hao kuguna kulizua mjadala mkubwa, jambo ambalo Idris aliona ni cha kawaida na kudai kuwa yupo kazini na kama kuna watu wengine nao wapo kazini kumwangalia maungo yake, basi imekula kwao.

“Jamani mimi niko kazini. Kama kuna mtu anajadili na maungo yangu, atakuwa naye yupo kazini na anajisumbua tu,” alisema.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad