Wanawake Kuandamana Kuhusu Madai ya Ubakaji Katika Hospitali Kenya

Wanawake Kuandamana Kuhusu Madai ya Ubakaji Katika Hospitali Kenya
Kundi la wanawake nchini Kenya limeandaa maanadamano hii leo ya kuishinikiza serikali kuchukua hatua kuhusiana na madai kuwa akina mama waliojifungua wamekuwa wakidhulumiwa kingono katika Hospitali kuu ya Taifa, Kenyatta National Hospital.

Maandamano hayo yanatarajiwa kufanyika wakati ambapo pia usomwaji wa ripoti ya uchunguzi uliyoagizwa na waziri wa afya nchini humo utakuwa ukifanyika.

Waziri wa afya nchini Kenya Dkt Cleopha Mailu aliagiza uchunguzi kufanywa katika hospitali ya kitaifa ya Kenyatta baada ya wanawake waliojifungua kudai kwamba wanadhalilishwa kingono.

Taarifa zilizoenezwa kwenye mitandao siku ya Ijumaa zinadai kina mama waliojifungua wamekuwa wanashambuliwa na baadhi ya wafanyikazi wakati wakienda kwenye chumba cha watoto wachanga kuwanyonyesha watoto wao.

Wanawake 100 hujifungua kila siku hospitali ya Kenyatta
Wanaotuhumiwa ni wahudumu katika vyumba vya maiti, wanaonyooshewa kidole pia kwa kutumia maiti kuwashutua akina mama waliojifungua katika hospitali hiyo.

Kundi hilo la wanawake linaloandamana leo katika mji mkuu, linasema dhamira yao kuu kumiminika barabarani ni kutaka mabadiliko yafanyike, na kwamba usalama wa wanawake ni jambo linalopaswa kutiliwa umuhimu.

Hospitali ya taifa ya Kenyatta, Nairobi huwahudumia kina mama takriban 100 wanaojifungua kila siku.

'Limekuwa likiendelea kwa muda usiojulikana, na ni lazima liishe'.
Mildred Atty, Moja ya waandalizi wa maandamano
Watoto waliozaliwa huwekwa chumbani ghorofa ya kwanza nao wanawake kwenye wodi za kujifungulia kwenye ghorofa ya chini.

Maswali sasa yameanza kuulizwa kuhusu muundo na mpangilio wa vyumba katika hospitali hiyo ambao huwalazimu kina mama waliojifungua kupanda ngazi au lifti kwenda kuwanyonyesha watoto wao, ikizingatiwa kwamba baadhi hujifungua kupitia upasuaji.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad