Kundi la wanamgambo wa Kiislamu la Boko Haram limerusha mkanda wa video mpya unaoonyesha wanafunzi kumi na nne wasichana waliotekwa katika mji wa Chibok, Kaskazini mwa Nigeria, mwezi April 2014.
Mmoja kati ya wasichana hao ameongea kwa niaba ya wenzake namnukuu “Sisi ni wasichana wa chibok, kwa uwezo wa Mungu, hatutorudi, tunawasikitikia wasichana wenzetu ambao waliamua kurudi nyumbani. Mungu aliwabariki na kuwaleta kwa Khalifa (sehemu takatifu) lakini badala yake, waliamua kurudi katika uovu “
Huu ni mkanda wa kwanza wa video unaowaonesha wasichana wa Chibok ukiachilia mbali uliotoka mwezi May 2017, ulioonyesha msichana mmoja akisema yeye ni miongoni mwa wanafunzi 219 waliotekwa katika mji wa Chibok, alionekana ameshika bunduki na yeye pia alikataa kurudi nyumbani.
Hakuna kitu kinachoonyesha muda au mahali video hiyo iliporekodiwa, wala kuonyesha kuwa wasichana hao wamelazimishwa kufanya hivyo.
Msichana huyo pia amewaambia wazazi wake: “mnapaswa kutubu, moto wa Jahannamu ni makazi yenu ikiwa hamtotubu, kwa sababu Allah ametuumba ili tumuabudu”.
Pia amemshukuru kiongozi wa kundi la Boko Haram, “baba yetu Abubakar Shekau, ambaye alitutoa huko, tunaishi katika faraja , Abubakar Shekau ni kiongozi wetu”.
Shekau ambaye alidaiwa mara kadhaa kuwa amefariki, pia ameonekana kwenye video hiyo, akirusha risasi kwa ktumia bunduki kubwa ya kivita kabla ya kuongea ambapo aliongea kwa dakika 13.
Jumla ya wasichana 276 walikamatwa mwezi April 2014 katika shule yao ya sekondari huko Chibok, katika jimbo la Borno, na kusababisha manung’uniko kwa watu wa mataifa mbalimbali
Wasichana Waliotekwa na Boko Haram Wagoma Kurudi Nyumbani
0
January 17, 2018
Tags