Wastara Afichua Siri Chanzo cha Ndoa Yake na Sadifa Kuvunjika "Mume Wangu Alitaka Hela za Michango"

Wastara Afichua Siri Chanzo cha Ndoa Yake na Sadifa Kuvunjika "Mume Wangu Alitaka Hela za Michango"
Msanii wa filamu bongo ambaye hivi karibuni amekuwa akipokea michango kutoka kwa watu mbali mbali kwa ajili ya matibabu, ameweka wazi moja ya sababu iliyofanya ndoa yake na kigogo wa CCM Sadifa Khamis kuvunjika baada ya muda mfupi.

Akizungumza na mwandishi wa www.eatv.tv, Wastara amesema mume wake huyo alionesha kutojali matatizo yake na badala yake kuweka pesa mbele, baada ya kudai risiti za matibabu aliyoenda kutibiwa India, kwa hela za michango ya watu mbali mbali, ili arudishiwe na bunge na ziingie mfukoni mwake.

Wastara amesema kitendo cha Sadifa kudai risiti hakikukifurahia, kwani pesa aliyokwenda nayo haikutoka mfukoni mwake, bali zilitoka kwa watu mbali mali wakiwemo Makamu wa Rais Mama Samia Suluhu, Msanii Alikiba, rafiki yake Sadifa na wengineo.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad