Watoto Uingereza Kuanza Kufundishwa zaidi Kukabiliana na ‘Likes’ za Mitandao ya Kijamii Kuanzia Shule za Msingi

Kamishna wa Elimu nchini Uingereza Anne Longfield ameweka msisitizo watoto kuanzia shule za msingi nchini humo kufundishwa zaidi kuhusu uelewa wa masuala ya digitali ili kuwasaidia kuepukana na shinikizo la mitandao ya kijamii.

Hii imetokana na uchunguzi uliofanywa nchini humo na kugundua kuwa watoto wengi chini ya miaka 13 kutokana na mitandao ya kijamii akili na muda wao hujikita katika kupata likes na kutengeneza mwonekano wao wanaotaka uonekane kwenye mitandao hiyo.

Uchunguzi huu umebaini pia kuwa matumizi yaliyokithiri ya mitandao hii kwa watoto yanawafanya wajishushe kwenye nyanja mbalimbali kutokana na watu wanao wa-follow kuonekana wako juu zaidi yao kwa namna tofauti tofauti husuani watu maarufu.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad