Waziri Mwakyembe Atuma Salamu za Rambirambi Kufuatia Kifo cha Mwanamichezo Athuman Chama

Waziri Mwakyembe Atuma Salamu za Rambirambi Kufuatia Kifo cha Mwanamichezo Athuman  Chama
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe amepokea kwa masikitiko taarifa ya kifo cha Mwanamichezo nguli Ndg. Athuman Juma Chama kilichotokea jumapili usiku tarehe 07 Januari, 2018 katika Hospitali ya Taifa Muhimbili jijini Dar es Salaam.

TAARIFA KWA UMMA

Akielezea kifo cha marehemu Chama, Dkt. Mwakyembe amesema kifo chake ni pigo kubwa kwa sekta ya michezo hususani mchezo wa mpira wa miguu nchini ambayo marehemu alihudumu kwa umahiri wa hali ya juu na kujijengea jina na heshima miongoni mwa vijana wapenda soka na Watanzania kwa ujumla.

Dkt. Mwakyembe ametoa pole kwa familia, Shirikisho la   Mpira wa Miguu nchini (TFF), Baraza la Michezo Tanzania (BMT), ndugu, jamaa, marafiki na wanamichezo wote nchini na kuwaombea Mungu awape faraja katika kipindi hiki kigumu cha msiba.

Kipindi cha uhai wake marehemu Ndg. Chuma (Maarufu kama Jogoo) alichezea vilabu vya  Nyamaume Football Club, Pamba ya Mwanza, Copu United, Mzizima United, Yanga na Timu ya Taifa (Taifa Stars) aliyoitumikia kwa juhudi kubwa kabla ya kustaafu kucheza soka mwaka 1988. Hadi anafikwa na umauti marehemu Chama alikuwa mweka hazina wa Chama cha Wanasoka Tanzania mkoa wa Temeke (SPUTANZA)

Imetolewa na:

Octavian F. Kimario

Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini

Wizara ya Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo.

09/01/2018.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad