Taarifa zilizotufikia ni kwamba Waziri wa Maji na Umwagiliaji Mhandisi Isack Aloyce Kamwelwe amezivunja Bodi za Wakurugenzi za Majisafi na Usafi wa Mazingira za mikoa miwili.
Bodi hizo ni za Jiji la Arusha yaani AUWSA na ile ya mkoani Musoma ya MUWASA na kwa mujibu wa taarifa hiyo iliyotolewa na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Profesa Kitila Mkumbo, Waziri Kamwelwe amevunja bodi hizo baada ya kutoridhishwa na utendaji wake.
Waziri wa Maji Avunja Bodi za Wakurugenzi Majisafi na Usafi wa Mazingira
0
January 19, 2018
Tags