Wizara ya Uchukuzi Yaomba Radhi Kuharibika Kivuko cha MV Magogoni

Wizara ya Uchukuzi Yaomba Radhi Kuharibika Kivuko cha MV Magogoni
Wizara ya Ujenzi, uchukuzi na Mawasiliano kupitia Wakala wa Ufundi na Umeme, wameomba radhi wananchi wanaotumia kivuko cha Mv Magogoni jijini Dar es salaam, kuwa na subira katika kipindiki hiki ambacho wanashughulikia tatizo lake.


Kwenye taarifa maalum iliyotolewa kwa vyombo vya habari, imesema kivuko hicho kimeharibika kutokana na kamba na nanga za maboti ya wavuvi kunasa kwenye mitambo ya kuendesa kivuko hiko, na kusababisha huduma kusimama kwa muda.

Kutokana na tatizo hilo Wizara imesema viuko vingine kama Mv. Kazi na Mv. Kigamboni vinaendelea na shughuli za kuvusha watu, huku ikiwataka wananchi wanaofanya shughuli zao za kibinadamu upande wa Kigamboni kutokufanya shughuli hizo karibu na maegesho ya kivuko ili kuzuia tukio kama hilo kujitokeza tena.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad