Yanga na Azam Zapelekwa Mikoani

Yanga na Azam Zapelekwa Mikoani
Mabingwa wa kwanza wa Kombe la Shirikisho nchini Yanga SC watasafiri hadi mkoani Mbeya kucheza na Ihefu FC katika hatua ya 32 bora ya michuano hiyo ya (ASFC), kati ya Januari 31 na Februari 1.


Yanga ambao walitwaa kombe hilo lilipoanzishwa upya msimu wa 2015/16, wamepangwa na timu hiyo ya daraja la pili ambapo mchezo huo utapigwa kwenye uwanja wa Sokoine jijini Mbeya.

Klabu ya soka ya Azam FC yenyewe imepangwa kucheza na Shupavu FC ya Morogoro ambapo mchezo huo utapigwa kwenye uwanja wa CCM mjini humo. Wakati huo Green Worriors waliowatoa mabingwa watetezi Simba SC wamepangwa kucheza na Singida United kwenye uwanja wa Azam Complex.

Timu za ligi kuu ni Mbao FC ambayo itacheza na Kariakoo United huku Majimaji Rangers itacheza na Mtibwa Sugar ya Morogoro. Maji Maji FC  wataikaribisha Ruvu Shooting huku Njombe Mji FC watacheza na Rhino Rangers.

Tanzania Prisons wataikaribisha Burkina Faso Uwanja wa Sokoine mjini Mbeya wakati Kagera Sugar watakuwa wenyeji wa Buseresere FC Uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba. Mwadui FC wataikaribisha Dodoma FC Uwanja wa Mwadui Complex, Shinyanga.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad