Yanga Yalalamika Simba inabebwa

Klabu ya Yanga kupitia kwa Katibu Mkuu wake wamelalamikia kutokuwepo na usawa kwa Simba na yanga katika matumizi ya viwanja vya Uhuru na ule wa Taifa.

Mkwasa amesema, Yanga kesho inatakiwa kucheza kwenye uwanja wa Uhuru mchezo wake wa ligi kuu Tanzania bara dhidi ya Mwadui FC ya Shinyanga wakati Simba wao watatumia uwanja wa taifa siku ya Alhamisi kwenye mechi yao ya ligi kuu dhidi ya Singida United hivyo amesisitiza kuwepo na usawa kati ya vilabu hivyo juu ya matumizi ya viwanja tajwa.

Kuna wakati bodi ya ligi ilitangaza kuwa, Simba na Yanga zitatakiwa kucheza mechi zao kwenye uwanja wa Azam Complex kupisha shughuli za kiserikali siku ambazo timu hizo zingeutumia uwanja wa Uhuru kwa mechi zao, badala yake yanga ilicheza azam complex mchezo wake dhidi Tanzania Prisons lakini mechi ya Simba ikachezwa kwenye uwanja wa Uhuru.

“Tunatambua kwamba uwanja wa Taifa ulikuwa katika matengenezo na haujatumika kwa muda mrefu lakini kwa sasa unaonekana umekamilika, tulijaribu kuomba tuweze kuutumia lakini tumekosa hiyo fursa na tumepata taarifa kwamba kuna baadhi ya mechi zitachezwa poale lakini sisi mechi yetu ya kesho (Jumatano) itachezwa uwanja wa Uhuru.”

“Tulitegemea tungeanza kucheza pale lakini tunakosa hiyo fursa sasa inatupa shida upande wetu tunaonekana kama hatupewi thamani au umuhimu.”

“Nakumbuka mechi yetu na Prisons yanga ilicheza Jumamosi, Simba wakacheza Jumapili lakini sisi tukacheza kwenye uwanja wa Azam Complex  Simba wakacheza uwanja wa Uhuru kwa hiyo sisi tukakosa hiyo fursa, hii ni mara ya pili inakuwa wenzetu wanaanza kucheza na Singida Alhamisi kwenye uwanja wa taifa sisi kesho tumeambiwa tunacheza uwanja wa Uhuru.”

“Sasa angalieni namna gani hakuna usawa katika mambo kama haya, sisi tunaomba kuwepo na usawa kwa sababu hizi timu zote ni za watanzania wazalendo, kama kuna haki basi itolewe kwa sawa kwa vilabu vyote kuliko kubagua kwamba timu hii inatumia uwanja fulani hii inakosa fursa.”
Tags

Post a Comment

4 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Hovyoo! Analia-lia kama mtoto mdogo!
    Kwani huo uwanja ni wa-TFF, wa-Simba ama wa-Yanga??
    Serikali ya CCM a.k.a. YANGA, ndio wanapanga kuhusu uwanja wao... hizo lawama hebu zipeleke kwa JPM anayo majibu yako, utafurahi mwenyewe na roho yako.
    Kama una-timu MBOVU hata mkicheza mbinguni MTAFUNGWA tu!
    Kuepuka yote hayo, hebu jengeni kiwanja chenu..........mfyuuuuuu

    ReplyDelete
  2. viongozi wa yanga wametaka usawa na maneno yao yana mantiki tokana na mechi alizozielezea sasa sioni ndugu yangu unapayuka kwa jambo gani hadi useme jenga uwanja wenu wakati samba pia hawana uwanja au mechi popote pale!!! kwa nini simba wasiende cheza mechi chamazi!!!!
    halafu tuone hiyo mechi popote !!

    ReplyDelete
    Replies
    1. Simba hawana kiwanja na hawajalalamika.
      Kwa hiyo hilo povu la Mkwasa kamtolea nani?? Mwenye uwanja (serikali), Simba au TFF? Hebu mtufafanulie hapo tu.......DAWA NI KUJENGA KIWANJA CHENU BASI.....vinginevyo, mtalalamika kila siku, mwenye chake ndio mpangaji........MPO

      Delete
  3. Kama ligi kuu Bara itaendelea hivi hivi yaani kukomalia rushwa na upendeleo na kuacha mshindi wa kweli apatikane kwa matokeo swaafi na halali ya uwanjani ushishangae kuiona yanga ikiwa miongoni mwa timu zinazohofiwa kushuka daraja na kunako uhai mtakuja kuyakumbuka maneno yangu. Yanga miaka nenda miaka rudi alishazoweya kubebwa. Chini ya utawala wa Malinzi yanga ilibebwa na kudekezwa mno. Wale simba walilia mpaka wakachoka. Malinzi aliapa yakwamba katika utawala wake simba hawezi kuwa bingwa na kweli ila makali ya dhambi za dhuluma yatakuadhibu ulie mdhulumu akishuhudia laivu. Simba iliporwa wachezaji wake na kusainishwa kwenye vilabu vyengine kwa nguvu. Simba ilinyimwa points ilizostahili kupewa. Ratiba ya ligi ipangwa katika kumuekea yanga mazingira mazuri ya ushindi nakadhalika nakadhalika. Sasa leo yanga kiasi waseme Simba wanabebwa kwa sababu ni mchezo wa yanga kubebwa.

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad