ACT-Wazalendo Wapongeza Ujumbe wa Maaskofu Katoliki

ACT-Wazalendo Wapongeza Ujumbe wa Maaskofu Katoliki
Chama cha ACT-Wazalendo, kimesema ujumbe wa Kwaresma mwaka 2018 uliotolewa na Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC) kuhusu masuala  ya kisiasa, kichumi na kijamii unaonyesha jinsi demokrasia inavyominywa nchini.

TEC imetoa ujumbe huo Februari, 2018 ulioandikwa na maaskofu wote 35 wa baraza hilo, wakiongozwa na Rais wake, Mhashamu Tarcisius Ngalalekumtwa upo katika kitabu cha kurasa 20 ikiwa ni maandalizi ya ibada ya siku 40, kipindi ambacho ni cha mfungo wa kukumbuka siku 40 za Kristo kufunga na kwenda jangwani.

Akizungumza na wanahabari  leo Februari 12, 2018 Katibu wa Itikadi na Uenezi na Mawasiliano wa chama hicho, Ado Shaibu amesema, “Tunawapongeza  sana viongozi wetu wa dini kwa kujitokeza waziwazi kuonyesha ugandamizaji wa haki unaoendelea nchini.”

“TEC kutoa waraka wa kiuchungaji ni kurasa mpya katika siasa zetu tangu uchaguzi mkuu wa mwaka 2015 umalizike.”

Katika ujumbe huo,  TEC wamezungumzia hali ya kisiasa na kusema uamuzi wa Serikali kuzuia, maandamano, mikutano ya hadhara ya vyama vya siasa ni kwenda kinyume cha Katiba ya nchi.

Shaibu ameitaka Srikali kuondoa zuio batili la vyama vya siasa kutofanya mikutano ya hadhara ya kuzungumza na wananchi.

Mbali na hilo, Shaibu ameiomba Serikali itoe taarifa ya uchunguzi kupotea kwa mwandishi wa gazeti la Mwananchi, Azory  Gwanda aliyefikisha siku 84 tangu kupotea kwake sanjari na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya Kibondo, Simon  Kanguye.

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Hao Maaskofu walikuwepo wapi wakati vitendo vya kifisadi vikikisiri nchini? Magufuli na serikali yake kuziba mianya yote ya mambo ya kipuuzi watu na baadhi ya taasisi wanakimbilia kuitaja demokrasia kama kisingizio cha kumpiga vita. Kuna ushahidi tosha yakwamba kuna baadhi ya watanzania wangetamani kuendelea na Serikali corrupt ili waendelee na dili zao kama kawaida kwenye taasisi zao.

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad