Afya ya Rugemalila, Sethi Yazidi Kuwa na Mashaka

Afya ya Rugemalila, Sethi Yazidi Kuwa na Mashaka
February 2, 2018 Upande wa utetezi umeieleza Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kuwa afya ya mmiliki wa IPTL, Harbinder Singh Sethi na mfanyabiashara James Rugemarila zinaendelea kuwa za mashaka.

Hayo yameelezwa na Wakili wa utetezi, Respicius Didas baada ya Mwendesha Mashtaka wa TAKUKURU, Leornad Swai kumueleza Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shaidi kuwa upelelezi wa kesi hiyo haujakamilika.

Wakili Didas amedai kuwa wakati afya za washtakiwa zikiendelea kuwa za mashaka wanauomba upande wa mashtaka ukamilishe upelelezi ambapo Wakili Swai alijibu kuwa ni kweli upelelezi unachukua muda mrefu ila upo katika hatua za mwisho na kinachochelewesha ni upelelezi mwingine kuwa nje ya nchi.

Hata hivyo, Rugemarila aliieleza Mahakama kuwa hajawahi kupelekwa Hospital ya Taifa Muhimbili kwa ajili ya matibabu, pia anahisi ana saratani kutokana na uvimbe alionao mwilini mwake.

Baada ya kueleza hayo, Hakimu Shaidi amesema mahakama hiyo haina mamlaka ya kutoa amri wakatibiwe nje ya nchi na alishatoa amri kwamba watibiwe Muhimbili na kama inahitajika wakatibiwe nje ya nchi serikali ndio itasimamia. Aliahirisha kesi hadi February 16,2018.
Tags

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Hawa jamaa kwanini kila kukicha madai yao wanalilia kwenda kutibiwa India? Huko India kuna nini?

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad