Chama tawala nchini Afrika Kusini, ANC kimeahirisha mkutano wa viongozi wa juu wa chama hicho uliotarajiwa kujadili hatima ya Rais Jacob Zuma.
Rais Zuma yupo katika shinikizo kubwa ambalo linatoka ndani ya chama chake ambalo linamtaka ajiuzulu kufuatai kashfa ya ufisadi.
Mkutano wa kamati kuu ya chama hicho NEC unatarajiwa kufanyika siku ya februari 17 na 18 kwa mjibu wa taarifa iliyotolewa na kiongozi wa chama hicho cha ANC, Cyril Ramaphosa.
Hata hivyo badala yake taarifa iliyotolewa na chama hicho imeeleza kuwa wamekuwa na mazungumzo yenye ufanisi mkubwa na rais Zuma.
Baadhi ya mitandao nchini humo imekuwa ikieleza Rais Zuma anajiandaa kuachia madaraka iwapo makubaliano yatafikiwa na pande zote mbili.