Kesi inayomkabili Muigizaji Wema Sepetu imeendelea ambapo Ofisa wa Polisi WP Marry ameieleza Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kuwa Wema alimwambia anatumia Dawa za kulevya aina ya Bangi kama starehe na sio kuuza.
WP Marry ambaye ni shahidi wa tatu ameyaeleza hayo wakati akiongozwa na Wakili wa serikali Costantine Kakula, mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu Thomas Simba.
WP Marry amedai kuwa Wema alimueleza maneno hayo hayo wakati walipokuwa njiani kuelekea nyumbani kwake kumkagua.
Amedai kuwa February 4, 2017 aliagizwa kumtoa Wema mahabusu na kwenda kumfanyia upekuzi nyumbani kwake akiwa na OC CID na Maofisa wengine wa Polisi.
Amedai kuwa wakiwa wanajiandaa kuondoka Central Polisi kuelekea kwa Wema Bunju Basihaya, wakiwa kwenye gari kuelekea huko alimuuliza Wema kuhusu tuhuma zinazomkabili kwamba anahusika na Dawa za kulevya au kutumia.
Amedai kuwa Wema alijibu “Sijishughulishi na kuuza ila ila natumia bangi kama starehe”.
WP Marry amedai kuwa baada ya kumuuliza Wema alimwambia mara yake ya mwisho kuvuta Bangi ilikuwa Jumatatu ambapo swali hilo aliulizwa February 4,2017.
Alieleza kuwa walipofika nyumbani kwa Wema waligonga geti na kufunguliwa na mdada wa kazi ambapo walivyoingia ndani walikuta kuna mdada mwingine wa kazi.
WP Marry amedai kuwa kabla ya kuingia ndani Wema aliomba kumpigia simu dada yake ili awepo wakati wa kufanya ukaguzi ambapo dada ake alifika na kujitambulisha kwa jina la Nuru Sepetu.
WP Marry ameeleza kuwa wakati Wema anampigia simu dada yake alitoka dada mmoja wa kazi kumfuata mjumbe ambapo alikuja naye na kujitambulisha kwa jina la Steven Ndaho.
Amedai baada ya dada yake Wema kufika alitaka kuwapekua kabla ya kuingia ndani ambapo Nuru aliwapekuwa wote kabla ya kuingia ndani.
Amedai baada ya kumaliza upekuzi walirudi Central polis, February 8,2017 saa nne asubuhi alipewa maelekezo na Inspeta Wille kwamba aende na Wema kwa mkemia kuu wa serikali kwa ajili ya kuchukuliwa sampuli ya mkojo.
Baada ya kueleza hayo, Hakimu Simba aliahirisha kesi hiyo hadi March 12 na 13, 2018 kwaajili ya kuendelea na ushahidi.
Askari Polisi: Wema Kaniambia Anatumia Bangi Kama Starehe
0
February 26, 2018
Tags