Askofu Kakobe Amuangukia Rais Magufuli Amuandikia Barua ya Kumuomba Msamaha

Askofu Kakobe Amuandikia Barua Rais ya Kumuomba Msamaha

Kamishna Mkuu wa  Mamlaka ya Mapato (TRA) Bw. Charles Kichere amesema Askofu Kakobe aliandika barua kwa Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. John Pombe Magufuli  na kuomba radhi kutokana na kauli yake ya kebehi pamoja na matamshi yake ya dharau kwamba ana pesa nyingi kuliko Serikali.

 Askofu Zachary Kakobe akiendesha ibada katika  Kanisa la Full Gospel Bible Fellowship katika mahubiri aliyotoa kwenye  Ibada hiyo  akisema  “Yeye ana pesa kuliko Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania”,

Kamishna Kichere ameongeza kwamba kufuatia Matamshi hayo  Mamlaka ya Mapato TRA iliamua kufanya uchunguzi kufuatia kauli yake  hiyo aliyoitoa  ,mnamo tarehe 24.01.2018 ili kujiridhisha kama mapato yake yanalipiwa kodi.

Baada ya Uchunguzi huo Mamlaka ya mapato TRA imebaini  mambo kadhaa kutokana na   kufanyika kwa uchunguzi huo kufuatia kauli   ya Askofu Zachary Kakobe;

Kamishna Kichere amesema uchunguzi umegundua Askofu Zachary Kakobe hana akaunti wala fedha katika taasisi yoyote ya fedha hapa nchini.

Aidha uchunguzi ulibaini kuwa Askofu Kakobe ni mmoja wa wasimamizi wakuu wa akaunti za kanisa (Signatories) zilizopo katika benki ya NBC zenye jumla ya kiasi cha shilingi 8,132,100,819.00, kiasi hiki cha fedha kimetokana na sadaka, zaka na changizo ambazo zinatolewa na waumini wa kanisa tajwa hapo juu, hivyo kwa mujibu wa Sheria hakitozwi kodi.

Aidha imegundulika kuwa Kanisa lilikwepa kulipa kodi kiasi cha shilingi 20,834,843.00 ambazo zilitokana na uwekezaji katika makampuni ya kukuza mitaji.

Kodi hiyo imelipwa baada ya uchunguzi na kugundulika kwamba Kampuni inayomilikiwa na watoto wa Askofu Zachary Kakobe ilikwepa kulipa kodi kiasi cha shilingi 37,280,030.00 ambazo zimelipwa baada ya uchunguzi. Kwa ujumla, kiasi cha kodi kilicholipwa kutokana na uchunguzi huu ni shilingi 58,114,873.00.

 Kamishna Charles Kichere amesema Kanisa  hilo linatunza kiasi kikubwa cha fedha kwenye ndoo na ‘majaba’ kinyume na taratibu za utunzaji wa fedha, lakini pia uwekaji na utoaji wa fedha nyingi kutoka benki haushirikishi vyombo vya ulinzi na usalama kwa ajili ya usalama wa fedha zenyewe na wahusika.

Pia ilibainika kwamba Kanisa halitengenezi hesabu za Mapato na Matumizi ya Fedha kitu ambacho ni kinyume na Katiba ya Kanisa pamoja na sheria za usimamizi wafedha ambayo imepelekea matumizi mabaya ya fedha za waumini kama vile safari za nje ya nchi ambazo zimedhaminiwa na Kanisa lakini wanaosafiri ni Askofu na familia yake.

Vile vile fedha za Kanisa zinatumika kujenga nyumba ya mke wa Askofu, kwa jina lake na wala si kwa jina la Kanisa, kitu ambacho ni kinyume na taratibu za Kanisa.

Kamishna Kichere ametoa wito kwa Taasisi zote za dini ambazo zinajihusisha na shughuli zozote za kiuchumi kulipa kodi stahiki na kwa wakati kwa mujibu wa sheria, kanuni na taratibu za kodi.

Pia amezitaka Taasisi zote za kidini kufuata katiba zao ikiwa ni pamoja na kutengeneza hesabu za mapato na matumizi.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad