Kamanda
wa Polisi wa Mkoa wa Mwanza, Naibu Kamishna (DCP) Ahmed Msangi, katika
taarifa aliyoitoa jana kwa vyombo vya habari, alisema mtuhumiwa alitenda
kosa hilo juzi majira ya saa 10 jioni katika maeneo ya mtaa wa Password
kata ya Nyegezi, Nyamagana mkoani hapa.
“Inasemekana
mtuhumiwa alikuwa akiishi jirani na nyumbani kwao mtoto. Inadaiwa kuwa
majira tajwa hapo juu, mtuhumiwa alifika nyumbani kwao mtoto na kumkuta
akicheza na wenzake kisha alimwita waende wote chumbani kwake.
Mtoto
alimfuata mtuhumiwa na kwenda naye chumbani na baadaye mtuhumiwa
alifanyia mtoto ukatili wa kumbaka na kumsababishia maumivu makali
katika sehemu za siri huku mtuhumiwa akimwonya mtoto kuwa asiseme kwa
mtu yeyote juu ya jambo hilo,” alisema DCP Msangi katika taarifa hiyo.
Msangi
alisema baada ya mtoto kufanyiwa ukatili huo, alikaa kimya bila
kumwambia mtu yeyote hadi mama yake aliporejea kutoka kazini.
Kamanda
Msangi alisema wakati mama yake akienda kumwogesha, ndipo alipogundua
kuwa mtoto amefanyiwa unyama huo kisha alitoa taarifa kituo cha polisi.
Alisema baada ya kutoa taarifa, polisi walifanya ufuatiliaji wa haraka hadi eneo la tukio na kufanikiwa kumkamata mtuhumiwa.
Kutokana
na kumkamata huko, DCP Msangi alisema polisi wako katika upelelezi na
mahojiano namtuhumiwa na kwamba uchunguzi ukikamilika, mtuhumiwa
atafikishwa mahakamani kwa hatua zaidi za kisheria.
Kuhusu mtoto huyo, Msangi alisema alipelekwa katika Hospitali ya Wilaya ya Nyamagana na kwamba hali yake inaendelea vizuri.