AU Yachukizwa Kuapishwa kwa Raila Odinga Yaitaka NASA Kuheshimu Matokeo

Mwenyekiti wa Tume ya Umoja wa Afrika (AU), Moussa Faki Mahamat amesema anafuatilia kwa karibu mabadiliko ya hali ya kisiasa nchini Kenya na ameonyesha kutofurahishwa na sherehe zilizoandaliwa na Nasa “kumwapisha” Raila Odinga kuwa “rais wa watu wa Kenya".

Mwenyekiti huyo alisema kumbukumbu zinaonyesha wa Ujumbe wa AU wa Uangalizi wa Uchaguzi wa Kenya uliongozwa na rais wa zamani Afrika Kusini Thabo Mbeki ulirejesha taarifa kwamba uliona uchaguzi ambao matokeo yake yalikubaliwa na Mahakama ya Katiba ya Kenya.

Mahamat amesema, “Kwa kuzingatia hali hiyo, na kwa mujibu wa vyombo vyote muhimu, hasa Mkataba wa Afrika juu ya Demokrasia, Uchaguzi na Utawala, Umoja wa Afrika unakataa vitendo vyote vinavyodhoofisha utaratibu wa kikatiba na utawala wa sheria.”

Mwenyekiti anahimiza wote wanaohusika kuacha vitendo viovu vinavyoweka uthabiti wa kisiasa nchini Kenya kuwa katika hatari. Anawahimiza wadau wote wachukue hatua kwa kuzingatia Katiba ya Kenya na maandiko mengine muhimu.

Kadhalika Mwenyekiti wa Tume anawahimiza watu wa Kenya kuendeleza kikamilifu njia sahihi za utawala wa sheria na kuimarisha taasisi zao za kidemokrasia, na kuachana na vitendo vingine vinavyoweza kudhoofisha utulivu wa nchi yao na maendeleo yake ya kijamii na kiuchumi.

Pia amesema Umoja wa Afrika uko tayari kusaidia njia yoyote inayoonekana kuwa sahihi ili kuondokana na mvutano wa sasa kwa misingi wa kuheshimu kanuni na utaratibu wa kikatiba na utawala wa sheria.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad