Baada ya Kuapishwa Kuwa Balozi wa Sweden Dk.Slaa Amwahidi Kutomwangusha Rais Magufuli

Baada ya Kuapishwa Kuwa Balozi wa Sweden Dk.Slaa Amwahidi  Kutomwangusha Rais Magufuli
IKIWA ni dakika chache baada ya Rais Dkt. John Pombe Magufuli, kuwaapisha Dkt. Wilbrod Peter Slaa kuwa Balozi wa Tanzania nchini Sweden na Muhidin Ally Mboweto kuwa Balozi wa Tanzania nchini Nigeria, Slaa amefunguka kuwa hatomuangusha Rais na badala yake atajituma kwa nguvu zake zote kulitumikia taifa kwa manufaa ya nchi.

“Kwanza nimshukuru Mwenyezi Mungu, pia nikushukuru Rais Magufuli kwa kunichagua kulitumikia Taifa, wewe unafahamu vigezo ulivyotumia kuniteua.

“Ninakuahidi nitafanya kazi yangu kwa moyo wangu wote, akili yangu yote na kwa nguvu zangu zote ili kujenga uchumi wa kati wa nchi yetu, Mwenyezi Mungu akinisaidia pia nikishirikiana na timu ya wote. Mimi katika siasa zangu sijawahi kutoa ahadi, lakini leo naweza kusema tu kwamba sitokuangusha,” alisema Dkt. Slaa.

Tags

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Eee Slaa. Najua ni mzee lakini. Whats next mzee.utaanzisha chama kingine au kuoa Mswedeni.

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad