Baba Diamond: Queen Doreen ni Mnafiki,nikifa asisogelee jeneza langu

Wasalaam
Baada ya Queen Darleen kumfumua Baba Diamond, Baba yake mzazi huyo na yeye amemlipua Queen Darleen. Zari, Wema na Mama Diamond watajwa. .
Akizungumza na online TV moja, Queen Darleen alipoulizwa kuhusu Zari alisema ndie mwanamke pekee wa Diamond aliyeonyesha kumjali baba yao akiwataka wamalize tofauti zao
.
"Zari ni wifi mwenye roho nzuri na ndiye mtu pekee aliyekuwa anatushauri tumjali baba (mzee Abdul) japo baba mwenyewe kuumwa kwake amekuwa kama mtoto…Kwa kweli kwa sasa siwezi kusema baba yangu ni Abdul, baba yangu mimi ni Nasibu…” alisikika Queen mbeleni katika mazungumzo hayo.
.
Baba Diamond alipoulizwa na GPL kupitia Amani kuhusu kauli ya Queen Darleen alijibu kumtaka Queen Darleen asimjue tena Kama baba yake mzazi
.
“Asisogelee hata jeneza langu, yeye si amesema baba yake siyo mimi, baba yake ni Diamond basi sawa. Hata mimi simtambui. Nikiumwa, nikifanya chochote simhitaji,” alisema baba Diamond huku machozi yakimtoka
.
“Yani kabla hajawa na hilo jina, alikuwa anakuja hapa, anapika na tunakula pamoja leo hii kweli anasema mimi nina akili za kitoto, kwamba nikiumwa nakuwa sina akili? Lini mimi niliumwa nikawa kama mtoto au sina akili?, Diamond pamoja na ustaa wake wote hajawahi kuniambia maneno mazito kama hayo, hicho kiburi anakitoa wapi mtoto wa kike?”
.
"Yule mtoto mbaya sana, Yeye ndiye alikuwa anakuja hapa anasema ooh… sijui mama Diamond ndiye anayemsababishia Diamond agombane na Wema…ooh… sijui mara hivi kumbe mnafiki mkubwa, Binafsi hata mimi Zari namkubali maana natambua ana moyo wa huruma na akili kuliko huyu Queen.”
.
Uamuzi aliochukuwa kwa binti yake huyo wa kumzaa .
“Nimezichoma kabisa moto picha zake. Siwezi kuwa na mtoto halafu akanikana hadharani. Acha na mimi nimkane hadharani, hana maana. Asinisaidie kwa chochote, sihitaji msaada wake kwanza,” alisema baba Diamond Akizungumza na Globalpublishers

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad