Baba Mzazi wa Akwilina aomba kuonana na JPM, amesema ana siku 4 hajaoga

Baba mzazi wa aliyekuwa mwanafunzi wa chuo cha usafirishaji NIT aliyefariki kwa kupigwa risasi February 16 mwaka huu maeneo ya Kionondoni Dar es Salaam amesema ana siku ya nne hajaoga kufuatia taarifa za kifo cha mwanae huku akisema amemsomesha Mtoto wake kwa kuuza vitu vidogovidogo kama kuku, mayai na maembe ili aweze kusoma.

Akizungumza Ayo TV na millardayo.com Mzee Akwilini Shirima amesema angekuwa na uwezo angeonana na Rais Magufuli ili amweleze suala hilo nakuomba Serikali kumsaidia kwa chakula na sehemu pakuishi. VIDEO:
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad