Babu Tale na Salam SK Wamekuwa Mameneja wa Hovyo Sana Wanaombebesha Diamond Mzigo wa Migogoro na Media

Wasalaam wana JF...

Ni ukweli ulio wazi vyombo vyetu vyote vya habari vinatabia zinazo fanana na vinatofautiana sana kwa kiasi kidogo sana vyombo vyote vinapenda kubembelezwa ,kuabudiwa,kusifiwa na kupewa kipaumbele...lakini pamoja na haya yote wasanii wetu walio wengi wameweza kutoboa akiweno Diamond Platinumz...
Tutakuwa waongo na wanafiki tukihindwa kujua kuwa ukubwa na alipofikia Diamond kwa sasa kumechangiwa sana tena sana na vyombo vya habari hivi ambazo muda mwingine tunaviona vya wanyonyaji au havitoi haki au vina watangazaji wenye chuki na Roho mbaya kwa wasanii wetu tuwapendao.

Lakini pamoja na mabaya mengi ya media hizi Diamond ameweza kufikia hapa na nina fikiri kabisa alikuwa na watu wanao jua zaidi kutatua migogoro na kuimaliza inapotokea na kizuri zaidi hawa Mameja wake wamekuwa nae siku nyingi japo si sana lakini hivi karibuni Diamond na WCB wamekuwa wakiandamwa na migogoro na media tena migogoro isiyopatiwa ufumbuzi kwa makusudi na wachochea migogoro wakuu wamekuwa ni Mameneja wake wakina Babu Tale na Salam Sk...
Diamond si mkorofi ni mmoja wa watu hummble sana,pamoja na matatizo yake yote lakini si mtu anayependa migogoro na watu bali ni maneneja wake ndio si watatuzi wa migogoro bali ni wachochezi wa migogoro na media.....

Diamond alikuwa na mgogoro na EATV/EARADIO jitihada zilifanywa hasa Fella kutatua huu mgogoro japo mgogoro huu ulikuwa ni wa watangazaji wa Planet bongo na Diamond kwa kuokoteza maneno ya vichochoroni....lakini pamoja na jitihada za Fella kutatua mgogoro huu Babu Tale na Salam hawakuwa tayari na wakaenda mbali zaidi kutopeleka nyimbo pale hata za wasanii wote wa WCB sasa mgogoro huu umegeuzwa wa WCB na EATV/EARADIO.

Sasa wameingia kwenye mgogoro na Clouds baada ya Mose iyobo kuwapiga wambea lakini hili limegeuzwa kama ugomvi wa Clouds na WCB na hii imechangiwa sana na Mameneja hawa wawili Salam na Tale maana kwakweli wana midomo mirefu sana na kibri kilichopitiliza na wameligeuza jambo lile kuwa anayetafutwa ni Diamond kushushwa baada ya Clouds fm kusema wamesikitishwa na wambea wao kutandikwa na Iyobo,najua Clouds wanacho hitaji ni kuombwa radhi na walitegemea ni Diamond,Tale au Salam ndio wajitokeze kuomba msamaha kwa Clouds saa hilo jambo halijafanyika.

Lakini pamoja na hayo yote nilitegemea Mamneja wa Diamond hasa Salam Sk wakimya na si wapiga kelele au kushutumu watu ooooh wanataka kumshusha Diamond,ooh wana chuki kitu ambacho pengine si cha uhakika bali ni hisia....kwakweli Maneneja wa Diamond wamekuwa watu wa kuendekeza migogoro na kumbebesha migogoro Diamond isiyo na tija......
Sioni sababu ya Salam kuanza kutamba na kutoa povu instagram kwa jambo pengine halipo kabisa maana hata dunia inajua kuwa ni vigumu sana kumshusha Diamond kwa sasa maana walishamuacha akapanda...

Kama ni swala la Iyobo kuwapiga wambea wa Clouds hayo ni maswala yanayo muhusu Iyobo na wale wambea waliotandikwa hivyo ni vyema na ni busara kwa mameneja kujiweka pembeni na jambo hilo kwanza ni jambo la wanawake hivyo si vyema kujihusisha nalo.

Pamoja na WCB kupanga kufungua vituo vyao vya radio bado kabisa vyombo vilivyopo vinahitajika sana tena sana kwa ustawi wa wa wasanii wa WCB hivyo ni vyema sana mameneja mkafanya jitihada za kutatua migogoro kuliko kuikuza.

Wasalaam

By Ruttashobolwa

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. dimondi si unafukuza kazi wote kwa mpigo.
    CEO HAPA KAZI TU.
    AU VIPI AFANDE SELE?

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad