Boby Wine Atoa la Moyoni Kuhusu Kifo cha Mowzey Radio

Boby Wine Atoa la Moyoni Kuhusu Kifo cha Mowzey Radio
Msanii Boby Wine wa nchini Uganda ambaye pia ni mbunge wa bunge la nchi hiyo, amesema kuna umuhimu wa wasanii na watu maarufu nchini humo kuwa na ulinzi wa kutosha, ili kuzuia mashambulizi yanayowatokea na kupelekea vifo vyao.


Akizungumza kwenye msiba wa msanii mwenzao wa nchini Uganda Mowzey Radio, Boby Wine amesema tukio la kupigwa ka Radio sio la kwanza kwa wasanii wa nchini humo, lakini hata hivyo hakuna mtu aliyekamatwa na kufikishwa kwenye vyombo vya sheria na kahi kutendeka, na badala yake wanazidi kushambuliwa.

Boby Wine ameendelea kwa kusema kwamba Radio hakuwa kamilifu kama binadamu wengine, lakini kitendo cha mtu kumpiga mpaka kumsabishia kifo ni kitu kisichovumilika.

“Sio tukio la mara ya kwanza, wala ya pili au ya tatu, Danz Kumapesa watuhumiwa hawajakamatwa, AK47 hawajakamatwa, sasa tunampoteza Radio, sisi sio perfect, lakini nafikiri tunahitaji ulinzi zaidi ili kitu kama hicho kikitokea tunajua tuna ulinzi na haki itatendeka”, amesema Boby Wine.

Taarifa zaidi kutoka nchini Uganda zinasema kwamba polisi wameifunga bar ambayo lilitokea tukio la kupigwa Radio, huku likiendelea kumsaka baunsa anayetuhumiwa kumpiga na kuwakamata tena wafanyakazi wawili wa bar hiyo, ambayo waliachiwa kwa dhamana.

Radio anatarajiwa kuzikwa kesho kijijini kwao nchini Uganda, baada ya mashabiki kuaga mwili wake kwenye uwanja.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad